Stori: Sifael Paul na MAKONGORO OGING’
Akizungumza kwa njia ya simu kwa zaidi ya saa moja mwishoni mwa wiki iliyopita huku akikanusha kukimbilia mafichoni baada ya kuondoka nyumbani kwake Tabata-Kimanga, Dar hivi karibuni, Mbasha ambaye pia ni mwimba Injili kama mkewe, alianika kila kitu akidai cha siri kwamba anajua anachezewa mchezo mchafu baada kuwepo kwa gogoro zito kati yake na mkewe hadi kutishia uhai wa ndoa yao.
ASIMULIA TUHUMA
“Tuhuma zilizoripotiwa na binti aitwaye... (anamtaja jina) ambaye kweli ni ndugu wa mke wangu (Flora) kwenye Kituo cha Polisi Tabata-Shule (Dar) si za kweli.
“Anayefanya mambo hayo yote ni mke wangu, anataka nipotee ili awe huru. Mimi najua hilo.”
KASHFA YA KUTENGENEZA
“Hii kashfa ni ya kutengeneza ili nipotee lakini sipo tayari kupata aibu, bora nijiue.
“Mke wangu amekuwa tatizo kwenye ndoa yetu.
“Kweli ndoa yangu na Flora ina matatizo lakini matatizo yetu ya ndani sana hakuwa na sababu ya ‘kuinjinia’ mpango mchafu wa kunimalizia gerezani mimi ili yeye aponde raha.
“Nyuma ya haya mambo kuna vitu mtu ukivisema ni aibu sana kwa upande wa pili. Lakini navijua.”
MKE ALIONDOKA NYUMBANI
“Mke wangu aliondoka nyumbani na kwenda kuishi hotelini. Hebu fikiria hapo. Mwanzo alianza kwenda ‘gym’ saa 11:00 alfajiri na kurudi saa 4:00 asubuhi. Pia saa 10:00 jioni aliondoka tenda kwenda gym akawa anarudi kati ya saa 3:00 hadi 4:00 usiku.
“Nilipomuuliza alinijibu kuwa ni kwa sababu anatembea umbali mrefu. Hebu ona sababu ilivyo dhaifu jamani! Hata kama ungekuwa wewe mwandishi, unaonaje?”
“Mimi ni mtu maarufu, ningetaka mwanamke ningepata, iweje nibake?
“Jaribu kufikiria, katika tatizo kubwa kama hili ambalo linaweza kunifanya nifungwe, nilitarajia mke wangu awe upande wangu, lakini cha ajabu yeye ndiye amekuwa nyuma ya adui zangu, niamini nini mimi zaidi ya yeye kuhusika na kuniangamiza?”
“Hausigeli wangu ni mzuri, kwa nini nisimbake yeye?”
AFUATILIA
“Nilipofuatilia niligundua tayari kuna tatizo kwenye ndoa yetu. Mdudu alikuwa ameingia ndani ya ndoa kwani hadi sasa mke wangu siishi naye. Anaishi hotelini.
“Anachokifanya mke wangu ni kitu kibaya mno. Alimtengeza yule binti ambaye nilikuwa namsomesha sekondari pale (anataja shule maarufu Dar), akampa semina ya kutosha kwamba aseme nimembaka ili nipate misukosuko na yeye awe huru.
“Kama hiyo haitoshi, akala dili na madaktari, wakafoji majibu ya vipimo vikionesha kweli yule binti ameingiliwa, sasa sijui kama vipimo vilioneshaje kama ni mimi.
“Ukweli ni kwamba siwezi kuvumilia kuona napandishiwa kizimbani kwa jambo la kutengenezewa.
“Napiga picha nitakapofikishwa mahakamani jinsi ambavyo vyombo vya habari vitakavyoandika na picha zangu kwa kesi ya ubakaji ambayo si ya kweli.
“Dah! Inaniuma sana. Mke wangu nimemfanyia vitu vingi sana. Hakustahili kunitendea ubaya huu. Alikuwa hafahamiani na mtu yeyote mkubwa. Mimi ndiye nimempeleka kwa watu wakubwa wakamsaidia sasa amenigeuka, siamini. Narudia tena, heri kufa kuliko fedheha hii,” alisema Mbasha kwa uchungu.
HAYUKO MAFICHONI
Kuhusu kuwa mafichoni, Mbasha alisema: “Sipo mafichoni, sijaambiwa na mtu yeyote nikatoe maelezo polisi. Nipo nimejaa tele, nikiambiwa nahitajika nitakwenda kutoa maelezo yangu kwani sijawahi kutenda kosa hilo na Mungu awe shahidi yangu.”
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Dar, Marietha Minangi alithibisha kuwepo kwa ishu hiyo na kwamba uchunguzi wa kina unaendelea.
Flora na Mbasha walifunga ndoa Agosti 22, 2002 hivyo mwaka huu wametimiza miaka 12 wakiwa pamoja ambapo mtoto wao wa kwanza anaitwa Elizabeth.
CREDIT:GPL
6 comments:
Walokole achene unafiki. Kazi yenu kidharau watu wasiyokuwa walokole na kujifanya kuwa mnamiliki funguo za mbinguni. Hapo angekuwa mlevi kabaka mgetukana sana. Bora mimi ninayekunya pombe inayoonekana kuliko ninyi wanafiki wakubwa mnaonyooshea watu vidole na kufanya uchafu kama huo gizani. Yani jianaume zima linasali kwa kulinalia na kutoa kamasi madhabahuni kumbe libakaji. Kama hili jianaume lingehojiwa litoe maoni kuhusu walevi lingetukana sana. Acheni kudharau imani za wengine.
Kama Flora kachora hii movie basi atakuwa ana dhambi nzito. Kama umemchoka mwanaume si unamwambia tu kuliko kumtendea huo unyama? Walokole acheni roho ya kutu. Mnapenda sana kuonekana watakatifu na kumbe wanafiki.
Inaonyesha kuna pepo kajiinua kwenye familia ya watu wa Mungu,na wameacha mwanya huo bila kukemea..lakini vipimo vya DNA havidanganyi na aliye mruhusu pepo huyo mchafu ataabika..nawasifu polisi kutoharakia jambo bila uchunguzi..lakini na vipimo viwepo bila kuchelewa..
Ndugu na marafiki wakaribisheni nyumbani kwenu, lakini SIYO kwenye ndoa yenu. Siri yenu ni ya watu wawili tu na siyo vinginevyo. Mambo ya ndoa yakianza kutoka nje na watu wa nje kuingia ndani ya ndoa yenu ni hatari sana. Ndoa yenu inaweza kusimama kama mtakapoyatambua hayo. Kama hamuwezi, ni bora muachane mapema maana mtakuwa mnapotezeana muda tu. Mimi ninaimani kuwa swala lenu ni dogo sana na kama kweli MNAPENDANA, ndoa yenu itasimama. Acheni vyombo vya habari.
Yani we anonymous wa tatu unachekesha kweli, eti "watu wa Mungu". Na wale wasiyokuwa walokole ni watu wa nani???????
hajabakwa mtu hapa ni ushetani umeingia hapa ndani, Na mara nyingi sana wakina mama tunapoolewa tunapenda sana kuwakaribisha wadogo wadada zetu kwenye ndoa zetu na isitoshe utoaji wa huduma zetu unasinyaa kiasi kwamba mdogo mtu anazidisha upendo wewe mwenye mali ukijikalia tu kwa kuzingantia una mhudumu basi ukihudumiwa vyote usilie tulia kama maji ya mtungi. Tuacheni kujisahau tufanye yale yaliyotuingiza kwenye ndoa.. Nsema hivi kwa sababu nimeshayaona mengi sana ya aina hii, na mara nyingine unaweza kusingiziwa tu kisa kwa sababu ya kuwa na huruma na upendo..
Post a Comment