ANGALIA LIVE NEWS

Monday, June 16, 2014

RAFIKI ZANGU WALITAMANI NIFIE JELA

Video Queen wa Bongo, Agness Gerald ‘Masogange’ akipozi.

Stori: Mwandishi Wetu

Video Queen wa Bongo, Agness Gerald ‘Masogange’ amefunguka kuwa kuna baadhi ya rafiki zake walifurahia alipokamatwa na mzigo wa matirio yaliyodhaniwa ni unga Mei, mwaka jana nchini Afrika Kusini.
Agness Gerald ‘Masogange’.

Akizungumza mitandaoni, mrembo huyo ambaye kwa sasa amehamishia makazi yake Johannesburg, Sauzi alisema: “Kuna marafiki zangu wengine walikuwa wanapenda nikae ndani, si unajua sisi hatupendani?

“Mimi naweza nikakupenda wewe ukiwa na kitu, lakini mimi nikipungukiwa na kitu fulani huwezi kuwa rafiki yangu tena sababu Agness kakwama kitu fulani, kwa hiyo atakuwaje rafiki yangu?
“Wengine walikuwa wakiongea Agness alikuwa anaringa bora aende jela.
”GREDIT:GPL

No comments: