Godfrey Mwita, Afisa Misitu wa wilaya ya Kilolo
|
UFISADI mkubwa
umeripotiwa kutokea katika msitu wa halmashauri ya wilaya ya Kilolo, mkoani
Iringa.
Baadhi ya
watumishi wa halmashauri hiyo (majina yao yanahifadhiwa kwasasa) wanatuhumiwa kuhusika
na ufisadi huo.
Taarifa za
uhakika na ambazo zimethibitishwa na baadhi ya maafisa wa halmashauri hiyo
(siyo wasemaji) zinaonesha kwamba watumishi hao wanahusika na uvunaji wa magogo
bila idhini ya halmashauri yenyewe katika msitu huo.
Magogo
yaliyovunwa kwa mujibu wa mmoja kati ya wanyetishaji wetu zinaonesha kwamba
yana thamani ya zaidi ya Sh Milioni moja. Mbao na mabanzi ni baadhi ya bidhaa
zilizotokana na magogo hayo baada ya kuvunwa.
Jitihada za
kumpata Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Rukia Muwango hazikuzaa
matunda na taarifa kutoka kwa mmmoja wa wasaidizi wake inaeleza kwamba yuko nje
ya nchi kwa matibabu.
Alipotafutwa
Afisa Misitu wa Halmashauri hiyo, Godfrey Mwita angalau azungumzie taarifa hiyo
hakupatikana pia na mpaka tunachapisha taarifa hii simu zake za mkononi
hazikuweza kupatikana.
Mtandao huu
unaendelea na uchunguzi wa taarifa hii na tayari ina jina la mtumishi mmoja
anayehusishwa na tuhuma hiyo.
Mara uchunguzi
huu utakapokamilika, taarifa hii tutaiweka hewani, endelea kutembelea blog hii
No comments:
Post a Comment