ANGALIA LIVE NEWS

Monday, June 23, 2014

Uhamiaji yakanusha kutoroshwa Meneja wa Tanzanite One


Afisa Uhamiaji wa mkoa wa Arusha Daniel Nanomba akikanusha vikali taarifa za aliyekuwa Meneja Mauzo wa kampuni ya Tanzanite One, Jaques Beytel anayedaiwa kutoroshwa.

Imeripotiwa kuwa, Afisa Uhamiaji wa mkoa wa Arusha, Daniel Nanomba amekanusha vikali taarifa kuwa aliyekuwa Meneja Mauzo wa kampuni ya Tanzanite One, Jaques Beytel ametoroshwa.

Nanomba anakaririwa kueleza kuwa Jaques alikamatwa na Maofisa wa Uhamiaji tarehe Juni 10 mwaka huu ili kupatiwa notisi inayomuamuru kuondoka nchini Juni 13.

Kwa mujibu wactaarifa ya Afisa huyo kwa vyombo vya habari, Jaques alisindikizwa na si kutoroshwa, hadi
mpaka wa Namanga na si uwanja wa KIA kama ilivyoelezwa na uamuzi huo ulizingatia taratibu zote za kisheria.
Jaques Beytel anayedaiwa kutoroshwa

Nanomba alisema kuwa raia huyo, "ambaye ni mzaliwa wa Afrika Kusini na alikuwa mfanyakazi wa kampuni ya Tanzanite One ambayo tumewaita na kuwaonya."

Afisa huyo amesema kuwa hawamzuii mwajiri yeyote anayeajiri mtu kutoka nje ya nchi lakini amewataka waajiri wahakikishe kuwa watu hao wana kibali cha kufanya kazi nchini, vinginevyo watachukuliwa hatua kali.

Nanomba alisema hadi sasa wamewachukulia hatua waajiri watano na katika kipindi cha mwezi Januari hadi sasa tayari wamefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu 35 katika mkoa wa Arusha huku nchi ya Kenya ikiwa inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wahamiaji hao.

Kati ya wahamiaji hao 35 wako raia wa kenya 13, Ethiopia wanne, Kongo 4, Ghana 4, Wadachi 3, Mmarekani mmoja na kutoka nchi nyingine.

Pia wako Watanzania waliochukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwaajiri watu kutoka nje wasiokuwa na vibali vya kukaa nchini. 
Chanzo:Wavuti

No comments: