ANGALIA LIVE NEWS

Monday, June 23, 2014

WEMA SEPETU ATOA KAULI YA UCHUNGU BAADA YA WATU KUMTUKANIA MAMA YAKE MZAZI


Wema Sepetu ameonekana kufungukia wale wanaomtukana kila siku na sasa kufikia hatua ya kumtukana hadi mama yake mzazi...

Kupita mtandao mmoja wa kijamii, Picha  moja  ya  mama  mzazi  wa  Wema  Sepetu  iliyotengenezwa  na  kuwa  CHAFU  ilitolewa  na  kisha  kuanza  kushushiwa  matusi  mazito...
 
Baada  ya  Picha  na  Matusi  hayo, Wema amefunguka kwa uchungu kwa kuandika: 

 "Dah...! Sijui hata niseme nini...! Ila si mlitaka kuniumiza... leo mmefanikiwa... nawapeni hongera.... Tena mmetisha haswa... Kila sjku huwa hata siumizwi na matusi yenu cuz naonaga kama ni mnajisumbua tu... Hakuna siku nimelia kwa uchungu kama leo...

"I min mnitukane mimi mpaka mchoke but leave my mum out of it... Kawakosea nini nyinyi mama angu mpaka mfanye hivyo... Mzazi nwenyewe ndo nimebakia nae mmoja tu... mnataka afe na yeye nibaki yatima sio... dah... leo mmeniweza... saana jamani... Basi naomba isifike huko... nina uchungu sana na mama angu ... nampenda sana mama angu ila naona mnataka kuniulia mama angu... 

"Picha halisi ndo hio hapo juu kweli mtu uende ukamfanyie hivyo mama wa mwenzako... una mama wewe.. au uliokotwa na hujui uchungu wa mama... dah... nime surrender leo.... hongera zenu narudia tena... mmeniweza leo.... dah...

"Mungu nipe nguvu ktk hili jamani... Kwani nilichokikosea haswa ni kitu gani mpaka iwe hivi . Nimekosa nini mimi yarabi toba.... Eeeh mungu... Dah... Ila nashkuru..." Ameandika  Wema  Sepetu  kwa  Uchungu

2 comments:

Anonymous said...

tuwekeeni haya matusi yutaone nakuyasome siyo eti mnatufanyia usanii na matusi hatuyaoni

Anonymous said...

Ushauri wa bure kwa wema sepetu kila unapoumia mshitakiye mungu na muachiye mungu afanye kazi yake atakulipia hapa hapa kwa wabaya wako na maadui zako wasio na nia njema na wewe na mama yako.
dua ya mtu anayezulumiwa daima haiendi bure kwa mungu na ukiona unaumia na wao pia wanaumia zaidi yako soma maandiko ya quran bibiye. na jambo la mwisho ni kwamba unapojitangaza umeumizwa ukae ukijua wao wanachekelea na wana taka respond yako waione na wanapoiona ndo WANAZIDISHA.so chungu sana kaa kimya muachiye mungu akulipiziye.

na pole sana kwa kutukaniwa mama yako na wewe kufanya fujo au kulipiza kisasa hakusaidi muachiye tu mungu japo kuwa najua unaumia. mungu mkubwa atakulipia wema, pole sana.

u.s.a