“Hao wanaopinga siyo wanachama hai, ni wale ambao hawajalipa kadi zao kwenye vikao halali hawaji, badala yake wanasemea pembeni.” Yusuf Manji
BEKI wa zamani wa Yanga, Bakari Malima amesema kama mwenyekiti wao, Yusuf Manji angeondoka madarakani, timu hiyo ingekuwa katika wakati mgumu wa ushiriki wa msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.
Mkutano Mkuu wa Yanga uliofanyika Jumapili iliyopita jijini Dar e Salaam uliamua kumuongezea Manji mwaka mmoja wa uongozi hadi Juni 15 mwakani utakapofanyika uchaguzi mkuu.
Malima alisema: “Kimsingi sisi ndiyo tuliomkubalia na kumuomba Manji aendelee kuiongoza Yanga kwa mwaka mmoja zaidi ili tujenge timu hasa katika kipindi hiki cha usajili, kwani akiondoka muda huu tutayumba katika kusuka timu.
“Tazama hapa tunaelekea katika usajili na kama tungeendesha zoezi la usajili ni wazi tungeharibu baadhi ya mambo ikiwemo kutosajili ipasavyo, hivyo Yanga wasilaumiwe kwa uamuzi huu kwani ni wa wanachama wote.”
Beki huyo za zamani wa kati, alisema watu wanaoibua maswali kuhusu uamuzi huo wanataka kuiona timu hiyo ikiingia katika mgogoro wa kiuongozi na kushindwa kufanya vizuri uwanjani.

No comments:
Post a Comment