ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, July 31, 2014

BOSI ADAIWA KUMKATA MAPANGA MFANYAKAZI WA NDANI

Msichana wa kazi za ndani, Fonolia Lembres (12) aliyeshambuliwa kwa mapanga na tajiri wake, Emmanuel Msovera.
Msichana wa kazi za ndani, Fonolia Lembres (12) amenusurika kuuawa na mwajiri wake aliyetambulika kwa jina la Emmanuel Msovera ambaye ni kondakta wa Hiace, baada ya kushambuliwa kwa kipigo na kukatwakatwa mapanga mwilini.Fonolia ambaye kwa sasa amelazwa katika Hospitali ya Mkoa Mount-Meru, jijini hapa, amejeruhiwa vibaya kwa kukatwa kiganja cha mkono wa kushoto na maeneo mengine ya mwili kisa kikidaiwa kuwa ni kutuhumiwa kuiba shilingi 30,000 za bosi wake huyo.
Hata hivyo, majirani na nyumbani kwa mtuhumiwa huyo wameeleza kuwa msichana huyo amekuwa akipigwa kama mbwa mwitu kila siku kiasi cha wao kumtaka mtuhumiwa amrejeshe kwao iwapo ameshindwa kukaa naye.
Akizungumza kwa tabu akiwa hospitali alikolazwa , mfanyakazi huyo wa ndani alilalamika kutoona vizuri kutokana na jicho lake la kushoto kupigwa ngumi pia maumivu makali ya mkono pamoja na sehemu zingine alizokatwa kwa panga na fyekeo.

No comments: