Advertisements

Sunday, July 27, 2014

MHE. OMAR MJENGA AFANYA KIKAO NA MKURUGENZI MKUU NHC BWN. NEHEMIAH MCHECHU NA MKURUGENZI MTENDAJI WA KAMPUNI YA UJENZI YA DAMAC, BWN.SONIL VOHOR

Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai, Mhe. Omar Mjenga, akifanya kikao nyumbani kwake na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), BW. Nehemiah Mchechu na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya ujenzi ya DAMAC ya Dubai, Bw. Sonil Vohor.
Kampuni ya DAMAC imekubaki kuingia ubia na NHC kwenye ujenzi wa nyumba za makazi na biashara, na hotel za nyota tano na kiwanja cha golf.
Mwezi huu Julai tarehe 17, DAMAC walifanya ziara Tanzania kupata taarifa muhimu (fact finding mission). Mwenyekiti wa DAMAC Bw. Hussain Sajwan, atafanya ziara Tanzania mwezi Septemba 2014.
Mazungumzo yakiendelea.
Bw. Sonil Vohor (kulia), Mhe. Omar Mjenga(katikato) na Bw. Nehemiah Mchechu (kulia) katika picha ya pamoja.

No comments: