ANGALIA LIVE NEWS

Friday, July 4, 2014

OMBI KWA TUME YA UCHAGUZI DMV

Watanzania wa DMV tunajuwa kuna uchaguzi wa Jumuiya hapo Tarehe 9 August. Kama kawaida ya uchaguzi lazima kuwe na wakuchaguliwa na wachaguaji. Tunawashukuru kamati ya Uchaguzi na Uongozi unaomaliza muda wake kwa kuiendelezea hii Demokrasia .

OMBI ni kwamba kamati ya uchaguzi imeongeza muda wa tarehe ya uchaguzi mpaka August 9. WATANZANIA TUNAOMBA pia muda wa watu wa kujaza fomu za kugombea pia uongezwe.

Kwanini uongezwe.

  1. Ili kujaza nafasi ambazo hazina wagombea.
  2. Ili kuweza kuchagu. Kuna nafasi ambazo zina mgombea mmoja mmoja. Tunataka tuweze kuchagua, kwa hiyo kila nafasi lazima iwe na mgombea zaidi ya mmoja.


Kwa vile muda bado upo tunaomba mtoe nafasi kwa wana DMV waweze kuchagua viongozi. Tukiwa tumebakisha siku zaidi ya 30 hatunasababu ya kufanya uchaguzi huku nafasi nyingine zikiwa hazina Mgombea au zikiwa na Mgombea mmoja tu.

Uchaguzi bado kama mwezi hivi, Tunadhani itakuwa ni busara kwa Kamati ya Uchaguzi na Bodi Ya Jumuiya kulifanyia kazi hili.


Wenu Mwanachama Hai wa Jumuiya ya DMV,


IDUMU DMV

2 comments:

Anonymous said...

KATIBA YA ATC DMV HAIRUHUSU MAMBO YA "USWAHILI" KAMA HAYA,NDO MAANA IMEANDIKWA KWA LUGHA YA MKOLONI.MASWAAALI ? HAKUINA,TUNAENDELEA.

Anonymous said...

TAYARI KATIBA IMESHAVUNJWA TOKA MWANZO. HATA MGOMBEA URAIS LIBE HAKUWA MWANACHAMA MPAKA MWEZI ULIOPITA AKAWA MWANACHAMA ILI AWEZE KUGOMBEA. KAMA WALIWEZA KUVUNJA VIPENGELE ILI LIBE AGOMBEEE NI VIZURI PIA WAKAENDELEA KUVBUNJA VIPENGELE NA WENGINE PIA WAGOMBEE. TUME IMESHINDWA KULINDA KATIBA. TUENDELEE NA UPEPO.