Kama hewa ingekuwa inauzwa kama luku mbona wengi tungepumua kwa mahesabu kama wagonjwa wa pumu.
Ushaanza kusema nina maneno mengi kama vile nimebemendwa, aiiih! Jamani mbona hivyo?
Kwani kucheka ni kwa wenye meno tu na siye wenye mapengo tusicheke? Tuvumiliane basi mate yakiwarukia muone kama pafyumu.
Ushaanza maswali yako eti mate ya ugoro hayavumiliki? Jamani ina maana mbwia ugoro hatoi denda? Mmh! Hayo si yangu tuendelee na yetu.
Jamani mashositito mbona mwaka huu wangu, nani alikuambia kisasi cha kitu hulipwa kwa kitu? Au mmesahau akupigae shavu la kushoto mgeuzie na la kulia?
Basi mwanakwetu, juzi nimefuatwa wanguwangu na binti mmoja ambaye anajua shughuli yangu, alinimwagia machozi shuu, kulikoni? Si akanimwagia ya chumbani, mwaaa mwari likanishuka.
Moja alisema mumewe kukosa uaminifu, pili kushindwa kupatiwa penzi kamili. Aliendelea kusema kuwa mume wake pamoja na kuwa naye mbali na kukutana kwa muda mchache bado hakidhi haja kiasi cha kufikia hatua ya kuwa katika mateso, siku chache anazokuwa yupo nyumbani amekuwa akimuacha njiani.
Wazo lake kubwa lilikuwa ni kutafuta mtu wa pembeni ili awe akimsaidia pale mume wake anapokuwa nje kwa kipindi cha mwezi mmoja mpaka miwili.
Mmh! Mtoto wa kike ameyamwaga hadharani kwa kuwa mtu huyo wa kumtibu maradhi yake alishampata lakini alitegemea majibu yangu.
Haya, mmemsikia jinsi mtoto wa kike anavyoteseka. Nikamshauri asiwe mwepesi wa kutoa uamuzi bila kuangalia hasara zake, kwani ni kubwa kuliko faida, mwanamke unapoikosa haki yako ndani katu huwezi kuitafuta nje ya ndoa.
Unapopatwa na tatizo la mwenzio kutokukufikisha au mpenzi wako kuwa mtu wa kusafiri kila wakati, mwari wee nakuomba uwe mvumilivu na kulilinda penzi lako, najua unakuwa kwenye hali mbaya lakini ustahimilivu ni jambo la msingi sana.
Siku zote unapokuwa kwenye wakati kama huo, jiepushe na mawazo ya ngono au kuangalia picha za ngono ambazo zinaweza kukupa kishawishi.
Siku zote mawazo ya mtu huelekea pale anapofikiri, pia moyo una haki ya kutamani lakini wewe ndiye unayetakiwa kuuzuia.
Hakika ukiuendekeza utakupeleka kubaya.
Kitu kingine acha kuwa bubu kushindwa kumweleza ukweli mwenzako kuwa siku hizi hushibi.
Unatakiwa kuwa mkweli kwa mwenzako, kumueleza jinsi unavyoteseka kuachwa njia panda ili mtafute ufumbuzi wa tatizo lako. Huenda yeye huamini wewe unafurahia safari yenu kwa kuwa unakaa kimya.
Pia nwanaume nao lazima waelewe wake zao hakuna kitu walichokifuata kwao zaidi ya haki ya msingi. Jamani nasi tunahitaji kutoshelezwa!
Nani alikuambia punda au farasi anakufa kwa kupigwa mijeredi? Kupigwa kwake ndiko kunakomfanya aongeze mbio.
Pamoja na kufanya kazi nzito ambazo huchosha mwili wake lakini mwanaume unatakiwa upate muda wa kumpanda punda wako na kumpiga mijeredi, hutakiwi kumhurumia kwani kwake kipigo hicho ndiyo raha yake.
Mwanakwetu usikae kimya kwenye tatizo, zungumza ili muweze kuwekana sawa kila mmoja ajue kitu gani mwenzie amepunjwa. Jambo hili litawasaidia kumnyima nafasi shetani ambaye kishawishi chake kikubwa ni wanandoa kutoka nje.
Namalizia kwa kusema hakuna suluhu ya matatizo nje ya ndoa, zaidi ya kujidhalilisha kwani penzi la kweli limo ndani ya ndoa nje ya hapo ni kupotea njia. Jamani japo tunachelewa tubaki njia kuu mchepuko ni umalaya.
Yangu kwa leo ni hayo, tukutane wiki ijayo, ni mimi Anti Nasra, Shangingi Mstaafu. GPL
No comments:
Post a Comment