Advertisements

Wednesday, July 30, 2014

Shukurani kwa wana DMV kwa kuomboleza pamoja nami.

 Napenda kutoa shukurani za dhati , kwa wana DMV wote walioshiriana nami kwa namna yeyote ile kuomboleza kifo cha mdogo wangu Mpemdwa Focus D Maturlu.
Hakika umekuwa wakati mgumu sana kwangu. Kwa Kuwa nanyi  kume fanya wakati huu Kuwa na unafuu Mkubwa.
Wote walinipigia simu, walio nitembelea nyumbani, waliofika kwenye Ibada ya shukurani na wale walinipa Mchango wao wa rambi rambi. Mungu awabariki sana!

Napenda kutoa shukurani kubwa kwa Balozi wetu Mama Mulamula kwa kunipigia simu na kunipa pole, nilifarijika sana.
Nashukuru Raisi wa jumuia yetu bwana Idd Sandaly kwa kunipigia simu, kuja kuniona na Mchango wa Hali na Mali kweli amekuwa pamoja nami ktkt hali zote. Mungu atakulipa kwa wakati wake.
Namshuku sana mgombea uraisi wa jumuia yetu bwana Liberatus Mwang'ombe kwa kunipigia simu, na Mchango wake wa Hali na Mali Mungu akubariki.
Kwa namna ileile nashukuru mama Moshi mgombea naibu raisi wa jumuia, ubarikiwe !

Mwisho, nawashukuru sana wana Habari wetu wote kwa ushirikiano Mkubwa walionipa, Asante sana.
Sitawasahau watumishi wa Mungu wenzangu hapa DMV. Bwana awabariki na kuwaona Ktk kazi hii nzito tuliyopewa na Mungu.

Kwa namna ya pekee nashukuru Apostle Baraza, Rev Igogo na Rev Mbatta kwa jinsi walivyo simama nami Ktk msiba huu. Ni Mungu peke yake atakaye walipa. Jina la Bwana libarikiwe !!

Toka sakafu ya moyo wangu.

Bishop,Melchizedek D Maturlu
Mh Joshua Nasari (Mb) Arumeru Mashariki alishiriki ibada
 Watu mbalimbali walioshiriki ibada wakimpa pole Bishop Melchizedek Maturlu walipojumuika naye kwenye ibada ya kuomboleza kifo cha mdogo wake Mpemdwa Focus D Maturlu.
Watu mbalimbali wakijumuika na Bishop Melchizedek Maturlu wakiwemo wagombea wa uongozi wa Jumuiya ya Watanzania DMV.
kwa picha zaidi bofya soma zaidi


No comments: