Sunday, July 27, 2014

UCHAGUZI DMV, MASWALI MEPESI

Wana DMV ni wakati wa kufungua macho na masikio yetu, kwanza kabisa ni kuangalia sera za wagombea wetu ,Na Je wana simamia misingi ya Katiba, haki na maendeleo ya jumuia,
Libe naona Kama anachanganya mambo yanayohusu jumuia na mambo binafsi,
Anageuza mambo binafsi kuwa ya kijumuia ,Kwa mfano suala la kumwekea Mtu dhamana ni suala binafsi ,kwa sababu rafiki yako Akiwa na tatizo ukamdhamini,huwezi kusema ni moja ya mambo niliyo ifanyia jumuia, Je Libe anagombea ili kusimamia Katiba ya jumuia ya Watanzania DMV au matakwa yake binafsi,

Amekwisha sema anapingana na mchango wa 10$ kwa mwezi , hapo tayari anapingana na katiba ambayo Yeye mwenyewe Akiwa Kama mwanachama na Mtu ambaye anapaswa kusimamia na pia siku zote alikuwa wapi kuona 10$ ni mzigo, mpaka Uchaguzi ,

Libe aache kudanganya watu kuwa atafuta mchango wa 10$ kwa mwezi , ili aendeshe harambee analeta siasa sasa, kila mtanzania DMV anapaswa kujua harambee inataka Pesa Je atafanya harambee Mara ngapi kwa mwezi na kwa mwaka, kipi bora utoe 10$ kwa mwezi au ukatoe harambee kuanzia 200$-ni mambo ya hesabu tu, harambee ni shughuli inayofanyika pale inapobidi na huwezi kugeuza ndio chanzo cha mapato, Watanzania tunapaswa kuwa wabunifu juu ya mstakabali wetu,
Tim Libe kula kukicha ni malalamika tu, Kama huwezi kufanya kazi na balozi,board of trustee, sasa ukichaguliwa utafanyakazi na nani, na utaendelezaje jumuia maana jumuia inahitaji mshikamano na Maelewano ya pande zote, Mtu yo yote Yule anaye wagawa wana jumuia kwa misingi ya Udini au Ukabila hatufai,hapa Marekani sisi ni Watanzania sio waislam ,wakristo ,na wapagani
Na Kama umeweza kumsingizia Balozi utashindwaje kuwasingizia wagombea /Viongozi wengine, mpaka hapo umekuwa unaonyesha ni jinsi gani ulivyombinafsi na Mtu unayependa Makuu .
Libe sema umefanyia nini jumuia zaidi Kama jumuia ya wana DMV zaidi ya ushiriki wa mpira,
Nimesikitishwa sana na Libe Kwenda kumwona Mgonjwa na kubandika picha mitandaoni Hali akiijua kinachoendelea Kati ya Mke wa mgonjwa na Jamaa aliyewasindikiza, tutamwamini vipi Libe katika matatizo ya kifamilia haswaa Ndoa Kama kiongozi, Mtu ukiibiwa Bwana au mke atakusaidia kweli, kesi ya tumbili unampelekea Nyani,

Power of attorney , naomba tu kuwatahadharisha Watanzania wenzangu Hilo ni suala binafsi na wala haingii akilini Leo hii umpe Libe , au Viongozi wa jumuia kwa sababu kuna mambo mengi ya kiusalama unaweza kupoteza haki zako, kwa sababu linahusisha taarifa muhimu ambazo Mtu anaweza Tumia vibaya.

Namaliza kwa kusema Idd amekuwa msaada na mfano kwa Viongozi wa jumuia nyingine katika kuonyesha shughuli za jumuia zinafanywaje, jumuia nyingi zilikuwa hazijui juu ya kupata mikopo ya nyumba,kusafirisha maiti nyumbani kupitia Idd watu wamefaidika, siku zote ameonyesha kazi alizofanya kwa jumuia nzima.

Faustus