Ndugu
wana DMV wenzangu , uongozi Bora ni ule utakaoweza kuiweka jumuia yetu sehemu
bora na Kuiwekea heshima kama
ilivyofanywa kazi hiyo na Uongozi wa Kaka Iddi Sandaly. Kwa kifupi wote
tunajuwa sera za uongozi huu wa Mhe. Iddi zinaongozwa
na sera yake ya kwanza ambayo ni umoja kwa watanzania wote.
Nimesikiliza
Video ya Mhe. Libe, nimestuliwa kwa kusikia kwamba anakubali kuwa Jumuia yetu
ni Non-Profit kwa maana ni chombo ambacho si cha kibiashara. Lakini anaeleza kwamba
kwenye uongozi wake kuwa Jumuia itatoa mikopo kwa watanzania au wafanya
biashara wadogo wadogo. Non- profit hairuhusiwi kutoa mikopo hata biashara ya
kawaida hairuhusiwi kutoa mikopo (Loans).
Mikopo
inatolewa na Financial institution (banks). Sasa hii sera imekaaje wana DMV?. Ushauri wangu mimi naomba wagombea
watupe sera ambazo ni za kweli kuliko kusema vitu ambavyo havina ukweli au
ufafanuzi.
Mchango
wangu wa pili ni kuhusu Mhe. Libe alipogusia kuwa ataanzisha Nurse Association
ya watanzania. Kwenye hili naona mitafaruku miwili apa ambayo nadhani mimi kama mpiga
kura nadhani inaashiria kuwa hili lina longolongo.
Pili.
Je Kwanini tuangalie Nurses tu?. Najuwa hii ni professional ya Mhe. Libe,
lakini hapa DMV kuna watu ambao wanafanya
kazi za aina mbali mbali. Sidhani kama ni sahihi kuwasahau watu wa nyanja nyingine.
Nadhani uongozi bora ni lazima uhakikishe unawapa watu wote haki sawa, kuna
mafundi magari, madereva, ma bloggers , nk.
Najuwa
uongozi unaomaliza muda wake ukiongozwa na Rais na Mgombea wa muhula wa pili
Mhe. Sandaly, uliunda kamati ya Social and economic Empowerement. ambayo
imekuwa ikitupa matangazo ya Kazi, Mafunzo na mengineyo. Nadhani isingekuwa
sahihi kaka Sandaly kama
angesema anaanzisha Tanzanian Accountants Association , kwa vile yeye Sandaly
ni Accountant.
Naomba
kaka Libe awe anatupa sera zenye kuweza
kutolewa kwenye mabano.
Faustus
2 comments:
Muuliza maswali anaonekana ni mtu wa majungu na upeo wa kufiri na sawa na urefu wa maswali yake. Mdau nje ya Marekani
Waana DMV, tuweni makini tusije UUWA huu Muungano. Sisi kama sisi tunatakiwa kujiendeleza wenyewe kwa kila aina ya michango na sio kutegemea bure au vyama kuanzishwa ndani ya vyama!!sisi wenyewe ndio nguzo ya huu umoja. Asanteni.
Post a Comment