Advertisements

Saturday, July 26, 2014

WAZIRI MKUU MHE MIZENGO PINDA AANDAA FUTARI NYUMBANI KWAKE DAR ES SALAAM

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhad Mussa Salum alipowasili kwenye makaazi ya Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda (nyuma yao) Oysterbay jijini Dar es salaam kwa ajili ya Futari leo Jumamosi Julai 26, 2013. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na wa pili kulia ni Kamanda wa Kanda Maalumu ya Polisi ya Dar es salaam Kamishna Suleiman Kova
 Rais Kikwete na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali wakijumuika na waumini wengine katika Swala ya Magharibi katika  makaazi ya Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda Oysterbay jijini Dar es salaam alikoandaa Futari leo Jumamosi Julai 26, 2013
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiongea na baadhi ya waalikwa kwenye futari aliyoandaa, wakiwemo waigizaji Mpoki wa Ze Komedy, Stephen JB, na watangazaji wa redio
 Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali, Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda, Jaji Mkuu Mhe Mohamed Chande Othman na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam Ndg Ramadhani Madabida wakipakua futari
 Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba akijumuika na waalikwa wengine kupakua futari
 Mawaziri wakuu Wastaafu Mzee Cleopa Msuya na Jaji Joseph Sinde Warioba wakiwa wameketi pamoja na Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndulu (kulia, mwenye baraghashia) na Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw. William Erio
  Kamanda wa Kanda Maalumu ya Polisi ya Dar es salaam Kamishna Suleiman Kova (kushoto) akiwa na viongozi wa dini Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) la Ubungo jijini Dar, Lusekelo Antony 'Mzee wa Upako' (wa pili kushoto),  Rais wa shirika la kidini la Wapo Mission International Bishop Sylvester Gamanywa (kulia) na mashehe 
 Meza kuu ikifurahia jambo baada ya futari
 Meya wa jiji la Dar es salaam Dkt Didas Masaburi na Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi ya Chama Cha mapinduzi CCM (Taifa) Bw. Abdallah Bulembo wakiwa na waalikwa wenzao kwenye futari hiyo
 Sehemu ya waalikwa
 Wazee Mashuhuri wa mkoa wa Dar es salaam mezani pao
 Mufti wa Tanzania Sheikh Shaaban Issa Simba akiongoza dua baada ya futari
 Sehemu  ya waalikwa kwenye futari hiyo
 Rais Kikwete akiagana na mmoja wa wazee mashuhuri wa Mkowa wa Dar es salaam
 Rais Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilal na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakisalimiana na waalikwa baada ya kufuturu pamoja
 Rais Kikwetena  Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilal wakisalimiana na waalikwa 
 Rais Kikwetena Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakisalimiana na waalikwa baada ya futari
 Rais Kikwete akisalimiana na mchora katuni maarufu Ali Masoud 'Kipanya' huku Mrisho Mpoto akisubiri zamu yale
 Rais Kikwete akifurahi pamoja na waalikwa wenzie
 Rais Kikwete akisalimiana na mmoja wa wazee mashuhuri wa Dar es salaam
 Rais Kikwete akisalimiana na mwanamuziki Christian Bella
 Rais Kikwete akisalimiana na mwanahabari mkongwe Bw. Mwondosha Mfanga
 Rais Kikwete akisalimiana na mwanamuziki nyota wa kizazi kipya, Ommy Dimpoz

 Rais Kikwete akiongea na Mwana FA
 Rais Kikwete akisalimiana na mtayarishaji, Muongozaji na mwigizaji nyota wa filamu Kulwa Kikumba 'Dude
Rais Kikwete akiendelea kusalimiana na waalikwa wenzie

Mkono wa mwisho ni wa mtoto huyu aliyepata bahati ya kuagana na Rais Kikwete na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali baada ya futari

7 comments:

Anonymous said...

naulize nijuzuni wana dini je futari hii inasihi kwa mtu asiye muislamu? na la pili nini lengo la futari hii?

mkuu usizibe comment hii ni kutaka kujua tu na kuelima na wanaojua dini wakinijibu please usibaniye hii comment.

Anonymous said...

Mh. Pinda. You look good in that darzi. Convert to Islam my friend or just take your time to read about it.

Ramadhani mubaraq.

Anonymous said...

Hizi dini zilikuja na ukoloni,so mambo mengine ya kuswihi isitusumbue kwani utu wetu kwanza. Hapa Nampongeza Mh. Pinda kufanya tendo la ubinaadamu. Ubarikiwe sana baba yetu.

Anonymous said...

Mtoa maoni wa kwanza: Kwanza fahamu kazi ya dini katika jamii, hiyo itakusaidia kujibu swali lako. Pili, kumbuka mwezi wa Ramadhani ni mwezi wa toba.

Hakuna kitu kuswihi au kutoswihi kwa futari kwa wale wasio waislam. You need to read more about the function of religion in a society.

Anonymous said...

''On this day all things that are clean have been made lawful for you; and made lawful for you is the food of the people of the Book, as your food is made lawful for them. And lawful are the chaste Muslim women, and the women of the people of the Book who are chaste, (for marriage) and not fornication or liaison, if you give them their dowries. Useless shall be rendered the acts of those who turn back on their faith, and they will be among the losers in the life to come''.

Qur'an. Sura tul Al Maaida.

Anonymous said...

ftari iliyoandaliwa na asiye muislamu hasihi labda kwa maswala yake binafsi ya kisiasa au ya kibiashara.siku hizi kuna kuingia na gia ya watu kuftarisha waislamu na kupata manufaa yao binafsi.
watch them you will see them

Anonymous said...

5:5

Quran surat al-ma'idah 5:5

This day [all] good foods have been made lawful, and the food of those who were given the Scripture is lawful for you and your food is lawful for them. And [lawful in marriage are] chaste
anonymous wa July 27, 2014 at 2:42 PM usidhani watu wote haba mazoba zoba/vilazi hatujui dini yetu hii hapa tafsiri ya surat al-maidah na wewe umeitafsiri kwa maneno yako kwa kudhani kwamba wote hatujui dini yetu na quran yetu.

swali nataka kukuliza imekuwaje uzungumza habari za wanawake wakati umeulizwa swali kwamba je hizi iftar zinazo ftarishwa na wasio waislamu zina sini au laa?jibu swali usiwarukiye wanawake/wake, watoto wetu wa kike jibu swali na utoa aya sahihi si ubabaishaji wako wa shehuna.
na the people of the book si hawa wagalatia wazama hizi nasema hivi si kwa kashfa ila kwa vile wao wametoka mipaka ya kuwa ahlul kitaab,(people of the book) kwa wao kumuita yesu ni mungu/au ndo mtoto wa mungu.

so tafadhali sana mdau mwenzangu ukija hapa na aya zako make sure ni sahihi na unajibu mada na swali uliloulizwa si kutuleta aya ambazo unaziandika wewe mwenyewe.watu humu tuko makini sana usituone mbumbu buu mzungu wa reli.

nakupa hiyo hapo aya hapo chini kwa usahihi wake.

Surat Al-Mā'idah - سورة المائدة

5:5

This day [all] good foods have been made lawful, and the food of those who were given the Scripture is lawful for you and your food is lawful for them. And [lawful in marriage are] chaste women from among the believers and chaste women from among those who were given the Scripture before you, when you have given them their due compensation, desiring chastity, not unlawful sexual intercourse or taking [secret] lovers. And whoever denies the faith - his work has become worthless, and he, in the Hereafter, will be among the losers.


sijui ulikuwa unampigia nani vipande kwa kutoa hii aya na kutoka nje ya mada na kutokujibu swali uliloulizwa.au unawatamani sana wanawake wa kiislamu