Advertisements

Friday, August 1, 2014

CCM YASTUKIA USANII WA UKAWA

Chama Cha Mapinduzi kimewastukia Ukawa na kusema wanachofanya ni Usanii usiokuwa na tija mbele ya mambo ya msingi kwa Taifa la Tanzania, akizungumza na mwaandishi wa habari hizi Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye alisema hoja zote zinazotolewa na UKAWA zina majibu kwenye Sheria na Kanuni zinazoendesha Bunge la Katiba ,CCM pia imewashukia UKAWA kwa kuwatukana na kuwadhalilisha viongozi wa dini ambao wamekuwa wakisisitiza UKAWA kurudi Bungeni.

CCM yawaomba wabunge wa bunge la Katiba wanaotaka Katiba mpya waendelee na bunge litakapoitishwa tarehe 5/8/2014.

Kwa taarifa za ndani ya kikao hicho ,kikao kimeisha kwa kukubalina kutokubaliana ,pande mbili hizi zimekutana zaidi ya mara nne pamoja na kikao cha leo kilichoanza tangia asubuhi saa nne mpaka jioni lakini hakuna hata pande mmoja uliokubalina na mwenzake.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani Msajili wa vyama vya Siasa nchi anatarajiwa kuzungumza na waandishi wa habari kesho jijini Dar es Salaam.

1 comment:

Anonymous said...

Awamu ya pili ya lala salama katiba mpya inaanza, haya sasa mizengwe imeshaanza nafikiri tusipokuwa makini hizo siku7 mlizopewa zinaweka hela mifukoni bila ya kungamua lolote. Fuateni yale tume iliyoleta mezani kinachoogopwa nin nini???