ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, August 23, 2014

DJ JOE CAT DADDY AANDIKA HISTORIA MPYA KITUO CHA RADIO CHA WKYS KWA MARA YA KWANZA CHAPIGA NYIMBO KUTOKA AFRIKA, WIMBO WA DIAMOND UKIWEMO

Kituo cha Radio 93.9 FM WKYS jana usiku kiliandika historia kwa kupiga miziki ya Afrika ukiwemo my number one muziki wa Diamond aliyeshirikiana nae mwamumuziki mwingine wa Afrika Magharibi, Davido. Dj Joe Cat Daddy, Dj wa Kitanzania anayefanyakazi kwenye Radio hiyo ndiye aliyekua kwenye kipindi hicho kinachorushwa siku ya Ijumaa kuanzia saa 4 usiku ET mpaka saa 6 usiku. 

Kipindi kilianza kwa kupiga hip hop za Kimarekani mpaka ilipotimu saa 5 usiku ndipo alipoaanza kupiga nyimbo kutoka Afrika Magharibi wimbo wa Diamond my number one ukiwa wimbo wa pili na aliendelea na aina hizo ya nyimbo mpaka saa 5 na nusu usiku na kurudi tena kwenye hip hop za Kimarekani.

Dj Joe Cat Daddy juzi kati aliongea na Vijimambo na kusema sasa hivi ameishapata baraka zote toka kwa wakuu wake wa kazi kila siku ya Ijumaa mida ile ile na itimiapo saa 5 usiku atakua anapiga nyimbo toka Afrika zikiwemo nyimbo za Africa Mashariki hususani Tanzania kwa ajili ya kuporomoti nyimbo hizo hatimaye ziweze kupenyeza soko la Marekani. Team ya Vijimambo inampa pongezi zake kwa mikono miwili.

Kama una winbo ambao unafanya vizuri Tanzania na anga nyingine au unaweza kurekodi jingo hata kwa kiswahili na yeye ataitumia kwenye kipindi hicho kila Ijumaa Email yake ni djjoe202@gmail.com

No comments: