ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, August 9, 2014

SHAMIM MWASHA: Napenda mavazi ya Kiafrika zaidi!

Shamim Mwasha 

Ni miongoni mwa wanawake wachache wenye mchango mkubwa katika mitindo ya kisasa hususani kwa kina mama. Kupitia mtandao wake staa huyu mwenye taaluma ya habari amekuwa akitumia muda mwingi kuwafahamisha Watanzania maana ya fasheni kwa vitendo.

Shamim Mwasha ni mjasiriamali, mpiga picha na pia mmiliki wa mtandao wa mambo ya mitindo na urembo maarufu nchini unaofahamika kama 8020fashionsblog.com.
Ni miongoni mwa wanawake wachache wenye mchango mkubwa katika mitindo ya kisasa hususani kwa kina mama. Kupitia mtandao wake staa huyu mwenye taaluma ya habari amekuwa akitumia muda mwingi kuwafahamisha Watanzania maana ya fasheni kwa vitendo.


Muda mwingi amekuwa akifuatilia mitindo mbalimbali kimataifa na kuileta kwa Watanzania. Lakini kubwa zaidi amekuwa akihamasisha Watanzania kupenda kuvaa mavazi ya Afrika.


Na hii ndiyo sababu kubwa ya kuanzisha kampeni kubwa iliyofahamika kama ‘Back To Africa’(B2A), katika kampeni hii mavazi kama vitenge, kanga, batiki, vilemba vya Kinigeria vimekuwa vikihusika zaidi.


Akizungumza na Mwanaspoti wiki hii Shamim anasema unapokuwa Mwafrika huna budi kuonyesha uafrika wako kwa vitendo. Haileti maana kusisitiza uvaaji wa mavazi ya Kizungu huku yale ya Kiafrika yakiwekwa pembeni.


“Nimezaliwa na nimekulia Afrika, nina kila sababu ya kujivunia uafrika wangu. Kwa kuwa mavazi ni sehemu ya utamaduni wangu, naamini naeleweka zaidi pale ninapotupia Kiafrika,” anasisitiza.


Kwa muda mrefu amekuwa akionekana katika mavazi ya vitenge zaidi kwenye mitoko ya aina mbalimbali. Anasema hii ni kwa sababu vazi hilo linajitosheleza.


Mavazi ya Kiafrika yanajitosheleza. Kwa mfano vazi la kitenge, unaweza kuvaa kwenye mitoko mbalimbali. Ofisini, kwenye sherehe za kitamaduni lakini pia hata kwenye dhifa za kimataifa unaweza ukatupia kitenge na ukaonekana mwenye kuelewa suala zima la mitindo.


“Nathamini sana mavazi haya kwani kwangu hasa hii B2A ndio mpango mzima , kwa kifupi naamini kuwa kila mdharau kwao ni mtumwa na ndio maana niko mstari wa mbele kuhamasisha wanawake wenzangu kupenda kuvaa mavazi ya Kiafrika,” anasema.


Shamim anatajwa kuwa mwanzilishi wa mitindo hasa ya kitchen party kwa wanawake. Mara nyingi kile anachoanzisha ndio kinachoonekana kuvaliwa zaidi na wanaomfuatilia.


Je yeye hutumia urembo na mitindo kutoka kwa wabunifu gani hasa.


“Binafsi vitu vyangu na mikoba mara nyingi hupendelea vya wabunifu wa nje. Lakini linapokuja suala la mavazi na vipodozi natumia wataalamu wangu wa Kitanzania”. Baadhi ya wabunifu anaowatumia ni pamoja na Maznat na Eve Collection lakini kwa upande wa vipodozi anawatumia sana vya Shear Illussion na Glambox.
Credit:Mwanaspoti

No comments: