ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, August 26, 2014

UNAIKUMBUKA HII?

Five Tanzanian Shillings Banknote - Front Side
Habari zenu wadau, hebu jieleze unavyoikumbuka, ulivyoitumia na thamani yake ilivyokuwa, jitiririshe ili vijana waliokuwa hawakuiwahi kuitumia hii waitambue thamani yake

7 comments:

Anonymous said...

inanikumbusha mbali, shilingi tano ulikuwa anakula breikfast, lunch na dinner, wakati mwengine na chenji inabakia

Anonymous said...

hiyo hela kwanza kijana ukiwa nayo unatisha na si rahisi kuipata ==kama kwenu hamnazo..

Anonymous said...

hiyo hela zamani ni watoto wa wazito tuu walikuwa nazo hohehae ukiipata looooh siku hiyo hulali..

Anonymous said...

shilingi ilikuwa nauli ya wiki nzima ya daladala kwa sisi wanafunzi. duuh kweli tumemisi maisha ya mzee mwalimu yalikuwa pooooaaaaa

Anonymous said...

Hii ikiwa ni shilingi 5 ya noti, na ile ya silver yake ilikua inaitwa:
DALA, na ilipata jina hilo kwa sababu ilikuwa thamani yake wakati huo ni sawa na 1 US dollar.

Anonymous said...

Ya mwaka gani hiyo waziamani wenzangu

Anonymous said...

Naikumbuka sana Shilingi Tano ya noti. Enzi hizo, mshahara wangu wa mwezi ulikuwa Shilingi Mia Nne na Hamsini, na zilikuwa zinatosha mpaka unaweka akiba bank.