ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, September 30, 2014



 
EID UL’HAJJ - NORTH CAROLINA
Wanajamii wa North Carolina wanapenda kuwakaribisha nyote katika hafla ya Eid itakayofanyika Jumamosi asubuhi 7am-10am ya October 4th. Ratiba ni kama ifuatavyo.
~~~~~~~~
1)   Kuondoka millennium hotel 7am
         2800 Campus Walk Avenue, Durham NC 27705
 2)  Kuelekea msikitini kwa sala ya Eid 8am – 9am
         Parkwood site: 5122 Revere Rd, Durham NC 27713
3) Kuondoka msikitiki kuelekea kwenye hafla ya Eid 9am
Kwa ajili ya chai na Ibada.
9 Wickersham Dr, Durham, NC 27713
Kuanzia 9am mpaka 10am
10am msafara unarudi kuelekea hotel kwa kushiriki convetion ya DICOTA.
Kwa taarifa Zaidi wasiliana na:
Nassor Basalama (415)316-5247 au Hajj Abdallah (919)672-6063



MRATIBU WA MATAWI YA CCM MAREKANI LOVENESS MAMUYA AZINDUA SHINA JIPYA JIJI LA WASOMI TULSA, OKLAHOMA

Mratibu wa Matawi ya CCM Ndugu. Loveness Mamuya akisema machache wakati wa Uzinduzi wa Shina Jipya, Tulsa Oklahoma
Viongozi Wandamizi wa Shina la Jipya Kushoto Ndugu Emmanuel J Kamara na Katibu wake Ndugu Edgar Chiwanga
Mdau Akifurahia Kupata Kadi yake
Mjumbe Bryceson Motto akimwaga Sera kwa WanaCCM waliyojumuika
Kikao Kikiendelea

Mtandao wa Wanawake na Katiba Kuelimisha Katiba Inayopendekezwa

Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanawake na Katiba, Prof. Ruth Meena akizungumza katika Kongamano la Wanaharakati Kujadili masuala muhimu kwenye mchakato wa Katiba Mpya lililofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanawake na Katiba, Prof. Ruth Meena akizungumza katika Kongamano la Wanaharakati Kujadili masuala muhimu kwenye mchakato wa Katiba Mpya lililofanyika jijini Dar es Salaam.Mjumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba, Usu Mallya akizungumza katika Kongamano la Wanaharakati Kujadili masuala muhimu kwenye mchakato wa Katiba Mpya lililofanyika jijini Dar es Salaam. 
Mjumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba, Usu Mallya akizungumza katika Kongamano la Wanaharakati Kujadili masuala muhimu kwenye mchakato wa Katiba Mpya lililofanyika jijini Dar es SalaamKaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi akizungumza katika Kongamano la Wanaharakati Kujadili masuala muhimu kwenye mchakato wa Katiba Mpya lililofanyika jijini Dar es Salaam. Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi akizungumza katika Kongamano la Wanaharakati Kujadili masuala muhimu kwenye mchakato wa Katiba Mpya lililofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wakichangia mada katika Kongamano la Wanaharakati Kujadili masuala muhimu kwenye mchakato wa Katiba Mpya lililofanyika jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya wakichangia mada katika Kongamano la Wanaharakati Kujadili masuala muhimu kwenye mchakato wa Katiba Mpya lililofanyika jijini Dar es Salaam.Baadhi ya wanachama wa mtandao wa Wanawake na Katiba, TGNP pamoja na mashirika mengine yanayotetea haki za binadamu wakionesha mabango yenye jumbe mbalimbali juu ya mchakato wa Katiba inayopendekezwa. Baadhi ya wanachama wa mtandao wa Wanawake na Katiba, TGNP pamoja na mashirika mengine yanayotetea haki za binadamu wakionesha mabango yenye jumbe mbalimbali juu ya mchakato wa Katiba inayopendekezwa.

Watu 270 walazwa kwa kunywa togwa

Songea. Watu zaidi ya 270 wa Kijiji cha Litapwasi, Wilaya ya Songea, mkoani Ruvuma wamelazwa wengi wao wakiwa na hali mbaya katika Zahanati ya Lyangweni na Hospitali ya Misheni ya St Joseph, Peramiho baada ya kunywa togwa inayosadikiwa kuwa na sumu.
Tukio hilo lilitokea juzi mchana kwenye sherehe ya Kipaimara kwa mtoto Dickson Nungu (14) na kuzua hofu kubwa kwa wakazi wa kijiji hicho ambao wanaonekana kutoamini kilichotokea.
Wingi wa wagonjwa hao umesababisha zahanati hiyo kuelemewa na kiasi cha wengine kulazwa chini kwenye udongo, barazani na kwenye miembe wakisubiri kupatiwa huduma ya kwanza.

NYUSI AKUTANA NA WANAMSUMBIJI WA ZANZIBAR

Mgombea wa Urais wa Msumbiji kupitia chama cha FRELIMO Mh.Filipe Nyusi akipokea zawadi kutoka kwa Jumuiya ya watu wa Msumbiji wanaoishi Zanzibar.
Mgombea wa Urais wa Msumbiji kupitia chama cha FRELIMO Mh.Filipe Nyusi akizungumza na Wananchi wa Msumbiji wanaoishi Tanzania ambapo alitumia fursa hiyo kuwaomba wampigie kura kwani amekuja na mikakati mizuri ya kuboresha uchumi ambapo amedhamiria kuiondoa Msumbiji kwenye orodha ya nchi masikini,pia aliahidi kuwawezesha wakina Mama wa Msumbiji.
Wananchi wa Msumbiji wanaoishi Zanzibar wakisikiliza sera za Mgombea wa Urais wa Msumbiji kupitia chama cha FRELIMO Mh.Filipe Nyusi kwenye mkutano uliofanyika katika Hotel ya Zanzibar Beach Resort.
Mgombea wa Urais wa Msumbiji kupitia chama cha FRELIMO Mh.Filipe Nyusi akiongozana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya watu wa Msumbiji wanaoishi Zanzibar Asilia Lunji baada ya kumaliza mkutano wake wa kampeni kwa wapiga kura wanaoishi Zanzibar,Nyusi aliwaambia kuwa amefanya mkutano wa kwanza nchini Tanzania kwa sababu ya mahusiano mazuri baina ya Msumbiji na Tanzania
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiagana na Mgombea wa Urais wa Msumbiji kupitia chama cha FRELIMO Mh.Filipe Nyusi mara baada ya mgombea huyo kumaliza ziara yake Zanzibar.
Mgombea wa Urais wa Msumbiji kupitia chama cha FRELIMO Mh.Filipe Nyusi akiwaaga wananchi wa Zanzibar

Death announcement of former Diasporan Waceke Gitome, daughter of Pastor Gitome



We announce the sudden death of Joy Waceke Gitome Mbui, 31,formerly of Takoma Park, Maryland who passed away on Friday, September 12, 2014, at Nairobi Hospital.

Her father, Pastor David Gitome, went to visit her on Friday morning and during the visit she started coughing and looked quite ill (Her husband had been out of town and her young daughter was at a sleep over). Pastor Gitome took her to the hospital and upon arrival she was rushed to the ICU and diagnosed with severe Pneumonia. Her condition did not improve and shortly before midnight, the same day, Joy passed away peacefully, while holding both her parent’s hands and with a smile on her face.

Joy was laid to rest on Friday, September 19, 2014, in Nairobi. She was the beloved wife of Daniel Mbui and mother to Raquel Mbui, 4. She was the daughter to Pastor David Gitome and Mrs. Ada Gitome (formerly of Takoma Park, MD) and sister to Betty Mburu and Cecil Gitome.

Joy was known and loved by way too many people to enumerate. For all who knew her in Kenya and the diaspora, we would like to thank you for sharing your life with her and we are glad that you got to experience such a wonderful human being. We pray that you will celebrate her life by living your life to the fullest and while also preparing for eternal life. May God bless you!

You can Contact pastor Gitome on:

011 254 727 287 531

or Email-davidgitome@mail.com

Kura za hapana,siri zarindima bungeni

  Kampeni kali zatawala kwa wajumbe
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, jana walianza kupiga kura kupitisha Rasimu ya Katiba inayopendekezwa, huku ikifanyika kampeni kali kusaka theluthi mbili za wajumbe baada ya suala la Mahakama ya Kadhi kushindikana kuingizwa kwenye rasimu hiyo.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wajumbe watatu wanaowakilisha madherhebu ya dini na Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi, Andrew Chenge, walipewa fursa ya kuzungumza na kutoa kauli za kuwashawishi wajumbe wakubali kuipitisha rasimu hiyo huku suala kubwa likiwa ni Mahakama ya Kadhi.

KAULI YA PINDA
Kabla ya hatua ya kupiga kura kuanza jana alasiri, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alilazimika kutoa tamko la serikali kufuatia taarifa kwamba wajumbe hususan ambao ni waumini wa dini ya Kiislamu, wamedhamiria kuipigia kura ya `Hapana' rasimu hiyo.

Msimamo wa kuipigia kura za `hapana' rasimu hiyo ulitolewa mwishoni mwa wiki na baadhi ya wajumbe kwa nyakati tofauti bungeni wakati wakihakiki Rasimu ya Tatu iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi, Andrew Chenge, ambayo haijaingiza suala la Mahakama ya Kadhi kama ambavyo walitaka iwe.

Akitoa tamko hilo, Waziri Mkuu Pinda, alisema linafuatia kikao cha maridhiano cha pamoja kati yake na Kamati ya Uongozi wa BMK ambacho pia kiliwashirikisha pia viongozi wa dini za Kiislamu na Kikristo.

Kundi la Orijino Komedy wajiunga na Huduma ya Bima itolewayo na CRDB Microfinance Insurance Brokers

CRDB Microfinance Insurance Brokers ambao ni wakala wa bima za aina zote ikiwemo bima ya afya, moto, nyumbani na maisha wakishirikiana na kampuni zaidi ya kumi za bima nchini Tanzania,wamefanikiwa kuwapatia huduma ya bima ya maisha,mazishi na ulemavu wa kudumu Kundi la Wasanii wa Vichekesho la Orijino Komedy Company wao na familia zao kupitia African life Assurance (Tanzania) Ltd na bima ya afya wao na familia zao kupitia Kampuni ya AAR Insurance Tanzania.

CRDB Microfinance wanayo furaha kubwa kwa kuwapatia wasani hao huduma hiyo,kwani siku zote imekuwa ikifahamika kuwa msanii ni kioo cha jamii.Wasanii hao waliofanikiwa kujiunga na huduma hizo ni pamoja na Isaya Mwakilasa ‘Wakuvwanga’, Mjuni Silvery ‘Mpoki’, Lucas Mhuvile ‘Joti’, Alex Chalamila ‘McRegan’ na Kiongozi wa kundi hilo,Sekioni David na wengine ni Herry pamoja na Jonas.

Huduma hii inawahamasisha wasanii wengine,wanahabari,wanamitindo na watanzania wote wa hali zote kutembelea ilipo CRDB Bank tawi lolote nchini Tanzania,ili waweze kupata huduma nzuri ya na haraka ya bima "ndani ya mikono salama" .
Meneja wa CRDB Microfinance Insurance Brokers,Arthur Mosha (kushoto) akimkabidhi Kadi ya huduma ya bima ya maisha,mazishi na ulemavu wa kudumu Kiongoni Mkuu wa Orijino Komedy Company,Sekioni David (kulia) wakati wa hafla fupi iliyofanyika leo kwenye ofisi za CRDB Mikocheni jijini Dar.
Msanii Lucas Mhuvile ‘Joti’ akipokea kadi yake kutoka kwa Meneja wa CRDB Microfinance Insurance Brokers,Arthur Mosha.
 Msanii Isaya Mwakilasa ‘Wakuvwanga’ (kulia) akipokea kadi yake kutoka kwa Meneja wa CRDB Microfinance Insurance Brokers,Arthur Mosha.(wa pili kulia) ni Meneja Mkuu wa African Life Assurance,Nura Masoud na Kushoto ni Meneja Mkuu wa AAR Insurance,Majala Manyama.
Meneja Uhusiano wa CRDB Microfinance Insurance Brokers,Nargis Mohamed (kulia) akiwa na Msanii wa Kundi la Wasanii wa Vichekesho la Orijino Komedy Company,Mjuni Silvery ‘Mpoki’ katika hafla hiyo.
Picha ya pamoja.

TANZANIA KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA GIZ

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Michael John akitoa tamko kuhusu Siku ya Soko la Afya iliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa kushirikiana na Shirika la GIZ , itakayofanyika Oktoba 2 katika ukumbi wa Diammond Jubelee jijini Dar es salaam.
Naibu Meneja wa Miradi ya Afya wa GIZ Bw. Christian Ptleiderer akizungumza na waandishi wa habari kutoa wito kwa mashirika mengine yanayotoa huduma za afya nchini kuendelea kusaidia na kusambaza huduma zao katika maeneo yenye changamoto ya miundombinu na uhaba wa watumishi wa afya.Kulia ni Mtaalam na Mawasiliano wa shirika la GIZ nchini Bi. Vida Mwasalla.

Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imesema kuwa itaendelea kushirikiana na Shirika la Ujerumani la GIZ katika uanzishaji na uendelezaji wa programu mbalimbali za utoaji wa huduma za afya zinazolenga kupunguza vifo vya watoto walio chini ya umri wa miaka 5.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Michael John ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam wakati akitoa tamko kuhusu Siku ya Soko la Afya nchini iliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa kushirikiana na Shirika la Ujerumani la GIZ itakayofanyika Oktoba 2, jijini Dar es salaam.

Amesema Tanzania na GIZ zimekuwa zikishirikiana katika uboreshaji wa miradi mbalimbali ya afya kwa kusogeza huduma za afya karibu na wananchi kuanzia ngazi ya taifa, mikoa na Halimashauri za wilaya.

KIGWEMA, BEST NASSO: TUTAKUKUMBUKA SIDE BOY

Wasanii Best Nasso kushoto, Hamisi Kibiti ambaye ni Meneja wa Best Nasso na kulia ni msanii Kigwema kwenye picha ya pamoja wakiwa safarini kuelekea Lindi kwenye mazishi ya msanii mwenzao.
Mdogo wa msanii Side akiwa kwenye picha ya pamoja na Best Nasso, Kigwema na waombolezaji wengine mara baada ya kufika mkoani Lindi.

Wasanii wa muziki wa Bongo Fleva, Best Nasso na Kigwema wamefunguka kuwa daima watamkumbuka msanii mwenzao, Side Boy aliyefariki mapema jana kwa upungufu wa damu katika Hospitali ya mkoa wa Lindi.

Wakizungumza na mwandishi wetu kwa njia ya simu wakiwa njiani kuelekea msibani mkoani Lindi, wasanii hao walisema kuwa watamkumbuka marehemu siku zote kwa kuwa walikuwa marafiki wakubwa ndani na nje ya muziki na kuongeza kuwa ni msanii pekee aliyekuwa akiimba nyimbo zenye meseji zenye kugusa maisha ya watu kwa kujali zaidi ujumbe na siyo soko kama wanamuziki wengine.

“Hakuna neno tutakaloweza kusema kuelezea hisia zetu. daima tutamkumbuka Side Boy kama msanii mwenzetu, rafiki na kaka yetu. RIP”

(Habari/Picha na: Chande Abdallah/Gpl)

ONESHO LA SITE KUFUNGULIWA KESHO JUMATANO MLIMANI CITY,JIJINI DAR

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Saddick akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uwepo wa onyesho la kimataifa la utalii ‘Swahili International Tourism Expo’ (SITE) linaloandaliwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB),litakalofunguliwa rasmi kesho Jumatano katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City,jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB),Devota Mdachi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu onyesho hilo la kimataifa la utalii ‘Swahili International Tourism Expo’ (SITE) litakalofunguliwa rasmi kesho Jumatano katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City,jijini Dar es Salaam.

ONESHO la kimataifa la utalii ‘Swahili International Tourism Expo’ (SITE) linaloandaliwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) linafunguliwa rasmi leo (kesho Jumatano) katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City na litamalizika Jumamosi.

Tayari maandalizi yote kuelekea ufunguzi wa onesho hilo yamekamilika na kwamba watanzania wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuja kujionea vivutio adhimu wa taifa hili.

Shirika la Hifadhi ya Taifa (TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) pamoja na Shirika la Ndege la Ethiopia ndio wadhamini wa onesho hilo linalotarajiwa kushirikisha mataifa mbalimnali ulimwenguni.

MKUTANO WA JUMUIYA YA WATANZANIA SWEDEN NA KUMKARIBISHA BALOZI DORAH MSECHU

 Mama Dora Msechu Mheshimiwa Balozi wa Tanzania nchi za kinordic na Baltic alipokelewa kwa shangwe.
 Muziki hadi lyamba.
 Wadau wakiserebuka.
DJ Richie akitoa burudani.

DK.SHEIN AWAAPISHA WAKUU WAPYA WA WILAYA PEMBA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Amran Masoud Amran kuwa Mkuu wa Wilaya ya Wete Pemba katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo jioni,kabla ya uteuzi huo alikuwa Afisa Mdhamini Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Pemba
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Hemed Suleiman Abdulla kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Pemba katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo jiono,kabla ya uteuzi huo alikuwa Afisa Mdhamini Wizra ya Biashara,Viwanda na Masoko
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Jabu Khamis Mbwana kuwa Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Pemba katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo ,kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Wilaya Mkoani Pemba,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bibi SSP Sida Mohamed Himid kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini A Unguja katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo ,kabla ya uteuzi huo alikuwa Afisa Mdhamini Ofi ya Makamo wa Pili wa Rais Pemba
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Mohammed Faki Mohammed kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo ambapo anaendelea na kazi hiyo kwa kipindi kingine cha miaka mitatu,[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

Hajj the Divine journey


MEREMETA NA HASSANALI NDANI YA ZIMBABWE

MEREMETA NA HASSANALI launched in Harare on 26 Sept at the Zimbabwe Fashion Week regards

Festival Latinidades from Kali TV

Festival Latinidades Afro-latina is considered one of the biggest women festival in South America. This year Kali TV Brazil were able to capture some of the images from this wonderful festival. Enjoy the Festival.

Omar Kaseko Kali TV Founder/Producer http://www.kalitv.com 240-374-2192

RAIS KIKWETE AREJEA NCHINI KUTOKA MAREKANI KWENYE MKUTANO WA 69 WA UMOJA WA MATAIFA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadik  baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 30, 2014 akitokea Marekani alikohudhuria Mkutano wa 69 wa Umoja wa Mataifa.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na IGP Ernest Mangu, Mnadhimu Mkuu  wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi  Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Samuel Ndomba na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadik  baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 30, 2014 akitokea Marekani alikohudhuria Mkutano wa 69 wa Umoja wa Mataifa.