Advertisements

Friday, September 19, 2014

JESHI LA POLISI DODOMA WALIVYOIMARISHA ULINZI KUZUI MAANDAMANO YA CHADEMA


 Jeshi la polisi limeimalisha ulinzi katika maeneo yote ambayo yalitajwa na chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwa ndiyo watapitia wakiandamana kwenda kwenda Bungeni kuanzia saa 4 asubuhi ya leo

 Polisi wakiwa wamefunga kamba kati barabara ya mzunguko ya stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani na chuo cha biashara CBE  kwaajili ya kuwazuia waandamanaji hao waliopanga kwenda Bungeni
  Polisi wapanda farasi wakiimalisha ulinzi katika viwanja vya nyerere Squere ambapo Chadema wamepanga kuanzia maandamano kuelekea bungeni.
  Askali polisi wakiwafanya mawasiliano kwenye gari lao ambalo lilikuwa limepakia mbwa kwa ajili ya kuimalisha ulinzi katika viwanja vya Nyerere Dodoma kwa ajili ya kuwazuia waandamanaji wa Chadema walipanga kuandamana kwenda Bungeni.

Hivi ndivyo hali ilivyokuwa Dodoma kila kona ulinzi

2 comments:

Anonymous said...

tujiulize kwa nini wanakatazwa kuandamana?haki yao ya kikatiba iko wapi?
magamba kuna siku watatoka tu nchi ni ya wote

Anonymous said...

Kwa mwendo huu wa Chadema kuwa ni chama cha maandamano, CCM itatawala milele. .