Advertisements

Friday, September 19, 2014

MATUKIO KATIKA PICHA MBOWE ALIPOHOJIWA KWA SAA TANO, HUKU WAANDISHI WAKIPIGWA MABOMU KUTAWANYWA

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe Freeman Mbowe akiwasili kwenye makao makuu ya Jeshi la Polisi nchini,Mapema leo asubuhi tayari kwa kwenda kuhojiwa juu masuala mbalimbali likiwamo la kauli aliyoitoa kwenye Mkutano Mkuu wa chama hicho hivi katibuni, kuwa watafanya maandamano nchini nzima bila kikomo. 
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Freeman Mbowe akiwasili kwenye makao makuu ya Jeshi la Polisi nchini,Mapema leo asubuhi tayari kwa kwenda kuhojiwa juu kauli aliyoitoa kwenye Mkutano Mkuu wa chama hicho hivi katibuni,kuwa watafanya maandamano nchini nzima bila kikomo.
 Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),John Mnyika akizungumza na waandishi wa habari waliokuwepo kwenye eneo la makao makuu ya Jeshi la Polisi,juu ya kile kilichokuwa kikiendelea kwenye mahojiani katika ya Mwenyekiti wa Chama hicho na Jeshi la Polisi.Picha na Othman Michuzi.
 Makamu Mwenyekiti wa Chadema,Prof. Abdallah Safari na Wakili wa Chama,Wakili Mabele Marando wakiwasili kwenye Makao Makuu wa Jeshi la Polisi mapema leo.
 Baadhi ya Wachama na Wafuasi wa Chadema wakishangilia wakati Mwenyekiti wao akiwasili kwenye Makao Makuu ya Jeshi la Palisi leo.
Kamishna wa Polisi,CP Paul Chagonja akiwataka wanachana na wafuasi wa Chadema kuondoka kwenye eneo hilo kwani hakuna sababu ya kufanya fujo.
 Ulinzi mlali katika eneo hilo.
 Amri ikipita ya kuwataka wanachadema kuondoka eneo hilo.
 Askari akiwataka wanachadema kuondoka.
Huyu alikuwa akikaidi amri ya Jeshi la Polisi ilibidi aondolewe kwa nguvu.
 Ulinzi Mkali.  

No comments: