Advertisements

Monday, September 8, 2014

SKYLIGHT BAND YATIKISA JIJI LA DAR NYAMA CHOMA FESTIVAL


Sam Mapenzi, Joniko Flower na Hashim Donode wakiwapa raha mashabiki wa Skylight Band kwenye Nyama Choma Festival iliyofanyika miwshoni mwa juma katika viwanja vya michezo vya chuo kikuu cha Dar es Salaam.


Mashabiki wakiwa wameshona kwenye viwanja vya michezo vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika Nyama Choma Festival huku Skylight Band wakitoa burudani ya aina yake.

Aneth Kushaba AK47 akitoa burudani sambamba na Digna Mbepera kwa mashabiki wa muziki wa Live Band kwenye tamasha la Nyama Choma lililofanyika mwishoni mwa juma katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam UDSM.


Pale Aneth Kushaba AK47 (hayupo pichani) anapogusa mashabiki na uimbaji wake.




Ni hisia tu hakuna kingine....Skylight Band ni balaa.!



Nyomi la kufa mtu... hapa chezea Skylight Band ndio habari ya mujini kwa sasa.



Mashabiki wa Skylight Band wakijiachia kwa raha zao.


Mmoja wa mashabiki akiwa ameshika kiuno kuhamaki kwa kile anachokiona jukwaani kutoka kwa Skylight Band kwenye tamasha la Nyama Choma.


Aneth Kushaba AK47 akiwapa vionjo vya aina yake mashabiki wa Skylight Band kwenye tamasha la Nyama Choma.


Digna Mbepera wa Skylight Band akifanya yake jukwaani kwenye tamasha la Nyama Choma lililofanyika kwenye viwanja vya michezo vya Chuo kikuu cha Dar es Salaam-UDSM mwishoni mwa juma.



Sam Mapenzi akiporomosha mistari kwa mashabiki wa Skylight Band Nyama Choma Festival.


Ni burudani mwanzo mwisho.


Sony Masamba akiwachizisha mashabiki wa Skylight Band Nyama Choma Festival.

No comments: