Napenda kuufahamisha Umma wa Watanzania kuwa taarifa hizo zote zilizotolewa kupitia njia hizo ni za Uongo na uzushi mkubwa na zinalenga kuipotosha jamii kwani wafungwa hao wapo gerezani na wanaendelea kutumikia adhabu ya kifungo cha Maisha gerezani kwa mujibu wa Sheria.
Jeshi la Magereza nchini linatoa onyo kali kwa watu kujiepusha na uhalifu huo na linawataka wale wote wanaotumiwa ujumbe wa aina hiyo waepuke kuusambaza ujumbe huo kwa wengine bali waufute, kwani kuendelea kuusambaza ni kosa kisheria.
Aidha, Jeshi la Magereza linaendelea na uchunguzi wa kina ili kuwabaini wanaosambaza ujumbe huo likishirikiana na Vyombo vingine muhimu kwa lengo la kuwakamata wahalifu hao ili mkondo wa Sheria uchukue nafasi yake.
Imetolewa na;
Lucas Mboje, Mkaguzi wa Magereza,
Afisa Habari wa Jeshi la Magereza,
Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,
DAR ES SALAAM.
Septemba 8, 2014.
2 comments:
Mm mh hawa viongoz wetu ni mburulaz kweliii, watu wanauwa watu kila cku hawachukui sheria yeyote leo hii eti hawa ni wahalifu , shame on you guys rudini shule nyie ni viongoz fake
Kama hawa wameharibu watoto wetu,kamwe wasije uraiani. Nchi nyingi duniani zina sheria kali kuhusu ubakaji na kulawiti watoto,. So. No PAROLE PLEASE!!I'M A MOTHER,KWA KOSA HILI,NAKUBALIANA KABISA NA MAHAKAMA. LUPANGO MPAKA SIKU YA MWISHO!!!!
Post a Comment