Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akipokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mpya wa Rwanda hapa nchini, Mhe. Eugen Sayore Kayihura. Hafla hiyo fupi ilifanyika Ofinini kwa Mhe. Membe tarehe 08 Septemba, 2014.
Waziri Membe akizungumza na Balozi Kayihura mara baada ya kuwasilisha Nakala za hati za utambulisho. Katika mazungumzo hayo Mhe. Membe alimhakikishia ushirikiano Balozi huyo na kumwomba awe huru katika kutekeleza majukumu yake ya kazi wakati wote akiwa hapa nchini.
Balozi Kayihura akiwa na Maafisa Waandamizi wa Ubalozi wa Rwanda hapa nchini aliofutana nao. Katikati ni Bw. Sano Lambert na Bw. Ernest Bugingo.
Mhe. Membe akimsikiliza Balozi Kayihura wakati wa mazungumzo yao.
Mhe. Membe akiagana na Balozi Kayihura.
No comments:
Post a Comment