ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, September 6, 2014

WAZIRI WA UJENZI AFUNGA RASMI MAADHIMISHO YA SIKU YA WAHANDISI TANZANIA.

Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wahandisi mbalimbali hawapo pichani kuhusu umuhimu  wa Taaluma ya Uhandisi na Maendeleo nchini kabla ya kufunga mkutano  huo wa mwaka uliondaliwa na Bodi ya Usajili wa Wahandisi(ERB).
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wapili kutoka kulia akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi  Profesa Ninatubu Lema wakawanza kushoto pamoja na Mbunge wa  Tunduru kaskazini, Mheshimiwa Ramo Makani wakikagua baadhi ya kazi  zinazofanywa na wahandisi nchini.
Wahandisi zaidi ya 200 wakila kiapo cha Uhandisi mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Kisutu Waliyarwande Lema, huku viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akishuhudia tukio hilo.
 Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katikati akikagua moja ya mabanda mbalimbali katika maadhimisho ya Siku ya Wahandisi Tanzania.
 Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikabidhi zawadi ya kompyuta laptop  kwa mmoja kati ya wanafunzi wakike waliofanya vizuri katika masomo ya kihandisi nchini.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katikati akipewa maelezo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Baraza la Ujenzi  la Taifa (NCC) Dkt. Leonard Madaraka Chamuriho wakwanza kushoto  kuhusu kazi mbalimbali za Baraza hilo.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi mbalimbali katika picha ya pamoja na wanafunzi  waliofanya vizuri katika masomo ya Uhandisi nchini. Picha zote kwa Hisani  ya Kitengo cha Mawasiliano Serikalini–Wizara ya Ujenzi

No comments: