Advertisements

Friday, September 19, 2014

YANGA KUIVAA MTIBWA KESHO

Wachezaji wa Young Africans wakishangilia bao alilofunga Jaja katika mchezo dhidi ya timu ya Azam kwenye Ngao ya Jamii

Mabingwa mara 24 wa Ligi Kuu ya Tanzania bara timu ya Young Africans kesho watashuka dimbani kucheza mchezo wa ufunguzi wa VPL 2014/2015 dhidi ya timu ya wakata miwa wa Mtibwa Sugar kutoka manungu Turinani, mchezo utakaopigwa kwenye dimba la Uwnaja wa Jamhuri mjini Morogoro. 
Kikosi cha Young Africans kimewasili salama leo mchana mjini Morogoro kwa Bus la klabu na kufikia katika Hoteli ya kitalii ya Arc iliyopo eneo la nane nane ambapo wachezaji wote na benchi la ufundi wapo fit kuelekea kwenye mchezo huo.

Majira ya saa 10 kamili jioni kikosi cha Young Africans chini ya kocha mkuu Marcio maximo kimefanya mazoezi katika dimba la Jamhuri ambapo pia baadhi ya washabiki walijitokeza kwa wingi kushuhudia mazoezi hayo ya watoto wa Jangwani.

Wachezaji walifanya mazoezi kwa takribani saa moja ambapo mara baada ya mazoezi hayo, washabiki waliofurika waliomba kumsalimia Jaja kila mmoja kwa mukshika mkono huku kocha Maximo akisema vijana wake wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo.

"Tumejiandaa kuhakikisha tunapata ushindi, natambua Mtibwa wana kikosi kizuri kilichokaa pamoja kwa muda mrefu, lakini hicho hakiwezi kuwa kikwazo cha kututzuia kuibuka na pointi tatu dhidi ya wakata miwa" alisema Maximo. 

Aidha Maximo amewaomba wapenzi, washabiki na wanachama wa timu ya Young Africans kujitokeza kwa wingi kuja kuwapa sapoti vijana kwa kuwashangilia mwanzo mpaka mwisho wa mchezo.

Viingilio vya mchezo wa kesho ni Tshs 5,000/=

No comments: