Baadhi ya viongozi wa Wizara ya fedha wakifuatilia kwa makini mkutano uliokuwa ukiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile, ambapo ujumbe kutoka Tanzania ulikutana na Mwakili Mkazi wa Benki ya Dunia kwa Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Phippe Dongier hawapo kwenye picha kwa madhumuni ya kujadili masuala mbalimbali yanayohusu uchumi wa Tanzania. Kutoka kushoto ni Bw. John Cheyo ambaye ni Kamishna wa Bajeti, anayefuata ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar Bi Amina na wa kushoto kwake ni Bw. Said Magonya ambaye ni Kamishna wa Fedha za nje Wizara ya Fedha.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile alipokuwa akitoa msimamo wake kuhusu sera zinazopendekewa na Benki ya Dunia kwa mwakilishi mkazi wa Benki ya Dunia kwa Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Phippe Dongier.
Dr. Servacius Likwelile Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali akiwa pamoja na ujumbe kutoka Tanzania. Kutoka kulia ni Gavana wa Benki kuu ya Tanzania na kutoka kushoto ni Bi. Natu Mwamba Naibu Gavana wa Benki kuu ya Tanzania wakimsikiliza kwa makini Bw. Phippe Dongier ambaye ni mwakilishi mkazi wa Benki ya Dunia kwa Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi hayupo kwenye picha, alipokuwa akijibu hoja zilizowekwa mezani.
Bw. Phippe Dongier ambaye ni mwakilishi mkazi wa Benki ya Dunia kwa Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi alipokuwa akijibu hoja zilizotolewa na Dr. Servacius Likwelile Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali na kuahidi kuzifanyia kazi.
Picha zote na Ingiahedi Mduma – Washington DC.
No comments:
Post a Comment