Advertisements

Wednesday, October 1, 2014

KINANA ASHIRIKI KULIMA MUHEZA

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akielekea shambani kulima katika kijiji cha Kwemnyefu kata ya Mpapayu wilayani Muheza mkoani Tanga.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kulima na kupanda mahindi katika kijiji cha Kwemnyefu kata ya Mpapayu wilayani Muheza mkoani Tanga.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa shambani wakati wa kulima na kupanda mahindi katika kijiji cha Kwemnyefu kata ya Mpapayu wilayani Muheza mkoani Tanga.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakiongozana na vijana kutoka shambani baada ya kumaliza kupanda mahindi katika shamaba lililopo kijiji cha Kwemnyefu kata ya Mpapayu wilayani Muheza.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza jambo mbele ya diwani wa kata ya Mpapayu ndugu Richard Semgalawe mara baada ya kumaliza kulima ambapo aliwataka viongozi wa kijiji waache kuuza maeneo ya wanakijiji yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli za kilimo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi kadi kwa Bi.Halima Kibwana wa kata ya Kilulu wilayani Muheza.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa ofisi ya CCM kata ya Kilulu wilayani Muheza.
Wanachama na wapenzi wa CCM wakiwa wamejipanga barabarani kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kufungua shina la wakereketwa la Vijana wajasiriamali wa kata ya Kwemuyu.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kata ya Songa wakati alipotembelea kituo cha Habari za kilimo Songa ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa kilimo kimekuwa na kuongezeka na tatizo kubwa lililopo sasa ni masoko kwa mazao,Kituo hicho cha habari kitasaidia wananchi zaidi ya 26000 kwa mwaka.
Kisamvu kikiwa kimestawi vizuri nje ya kituo cha Habari za Kilimo kata ya Songa
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisomewa na Dk.Hilda Ponera taarifa za maendeleo ya uboreshwaji wa kituo cha afya cha Ubwari ambacho kipo kwenye utaratibu wa kupandishwa na kuwa hospitali ya wilaya.
Wodi mpya ya Wagonjwa katika kituo cha afya cha Ubwari
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipewa maelezo ya uboreshaji wa kituo cha Afya cha Ubwari kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri Ndugu Ibrahimu Matovu.
MNEC wa wilaya ya Muheza Mh.Laicky S. Gugu akisalimia wananchi walifurika kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Jitegemee wilayani Muheza mkoa wa Tanga.
Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Muheza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Jitegemee ambapo aliwaambia Vijana wajitokeze kwa wingi kwenye nafasi mbali mbali za uongozi kwenye chaguzi zinazofuata .
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutbia wakazi wa Muheza kwenye uwanja wa Jitegemee ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa kesi za masuala ya ardhi zinachukua muda mrefu sana kiasi cha kuchelewesha ufanikishaji wa maendeleo hivyo na kuzitaka mahakama za ardhi kushughulikia mapema.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza Ndugu Amri Kiroboti akitoa taarifa ya maendeleo ya utekelezaji wa miradi mbali mbali ikiwemo ya maji na umeme.
Wananchi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Jitegemee.
Ibrahim Mohamed almaarufu Ban Ki Moon akiuliza swali kuhusu kufungwa na kuondolewa gulio la Alhamis na Jumapili Muheza mjini

No comments: