Advertisements

Tuesday, October 14, 2014

Mfanyakazi wa UN afariki Ujerumani



Mfanyakazi katika kituo cha kuwahudumia wagonjwa wa Ebola.

Mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa aliyeambukizwa Ebola amefariki dunia katika hospitali moja nchini Ujerumani.

Madaktari katika hospitali ya Leipzig wamesema mtu huyo mwenye umri wa miaka 56, alifariki dunia mapema Jumanne asubuhi.
Mlipuko huo umeua zaidi ya watu 4,000 tangu mwezi Marchi, mwaka huu hususan katika nchi za Liberia, Sierra Leone, Guinea na Nigeria.

Shirika la Afya Duniani limeuelezea ugonjwa huo kama tatizo la dharura la kiafya kuwahi kuonekana katika maisha ya sasa ya binadamu. Marekani na Uingereza ni miongoni mwa nchi zilizoanzisha utaratibu wa upimaji afya za abiria kuhusiana na ugonjwa wa Ebola katika viwanja vya ndege.

Vifo vya Ebola Afrika
Kufikia tarehe 8 Oktoba


4,032

Vifo vilivyosababishwa na Ebola (idadi haijumuishi vifo nje ya Afrika)


Liberia 2,316


Guinea 778


Sierra Leone 930


Nigeria 8
Chanzo: WHO
Getty

Mtu huyo alikuwa akifanyakazi kama afisa wa afya wa Umoja wa Mataifa nchini Liberia- moja ya nchi zilizoathirika zaidi na maambukizi ya ugonjwa huo Afrika Magharibi- wakati alipoambukizwa Ebola.

Upimaji wa hali ya joto mwilini

Aliwasili Ujerumani Alhamisi iliyopita kwa ajili ya matibabu na aliwekwa katika kitengo maalum cha uangalizi.

"Licha ya matibabu ya kina na jitihada za hali ya juu za madaktari katika kumhudumia mwaajiriwa huyo wa Umoja wa Mataifa, hawakuweza kunusuru maisha yake kutokana na maambukizo makubwa". Imesema taarifa kutoka hospitali ya St Georg.

Wafanyakazi wa Afya wako katika hatari kubwa ya maambukizo.
Credit:BBC

No comments: