TAARIFA tulizozipata mchana huu kutoka mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, zinasema jeshi la polisi nchini limemkamata na kumfikisha katika mahakama ya kijeshi askari wake Pc.Godlisen anayetuhumiwa kumtumikisha katika vitendo vya ngono mwanafunzi wa kidato cha tatu wa shule ya sekondari Okaoni iliyopo wilaya ya Moshi.
Habari zinasema kuwa,askari huyo ambaye septemba 21 mwaka huu alimfungia kwenye nyumba ya kulala wageni mjini moshi mwanafunzi huyo na baadaye wawili hao kupata ajali mbaya ya pikipiki, aliumia kwenye moja ya bega lake na hivyo kushindwa kupelekwa kwenye mahakama ya kijeshi.
Kaimu kamanda wa liposi mkoa wa Kilimanjaro,Koka Moita, pamoja na kukiri kuwa wameanzisha uchunguzi kuhusiana na tuhuma hizo, alikataa kuweka wazi kama askari huyo amefunguliwa mashitaka ya kijeshi.
Kamanda Koka amewaambia waandishi wa habari leo kuwa, jeshi la polisi linafanya uchunguzi juu ya tuhuma hizo na kwamba kama itabainika,askari huyo atachukuliwa hatua za kinidhamu kabla ya hatua zaidi kuchukuliwa.
Pamoja na jeshi hilo kumfungulia mashitaka ya kijeshi askari huyo,taarifa kutoka kwa mmoja wa wazazi wa mwanafunzi hiyo zinadai kuwa,kuna juhudi za makusudi zinafanywa na askari wa jeshi hilo kutaka kukwamisha mashitaka ya kijeshi dhidi ya askari huyo.
Taarifa zinadai kuwa,polisi wa kituo kikuu cha polisi mjini moshi,wanajenga ushawishi kwa wazazi wa mwanafunzi huyo kutaka kulimaliza suala hilo kienyeji huku hali ya mwanafunzi huyo ikielezwa kuwa mbaya kutokana na miguu yake kuvimba.
Kwa taarifa zaidi endelea kutembelea mtandao huu wa
No comments:
Post a Comment