Advertisements

Thursday, November 27, 2014

BILEKU MPASI KUTOKA CONGO (DRC) NA MASHUJAA BAND KUFANYA ONESHO LA PAMOJA DISEMBA 12

Rais wa Band ya Mashujaa, Chalz Baba (kushoto), akitoa burudani mbele ya wanahabari Dar es Salaam leo, kuhusu onesho hilo litakalofanyika katika ukumbi huo.. Kutoka kulia ni Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia ya Mabibo, Joseph Emanuel na Ofisa Uhusiano wa Band ya Mashujaa, King Dodo la Buche. 
Ofisa Uhusiano wa Band ya Mashujaa, King Dodo la Buche (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu onesho hilo. Kulia ni Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia ya Mabibo, Joseph Emanuel na Rais wa Band ya Mashujaa, Chalz Baba. 
Meneja Matangazo wa Band ya Mashujaa, Maxmilian Luhanga (katikati), akizungumza katika mkutano huo. 
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia ya Mabibo, Joseph Emanuel (katikati), akizungumza katika mkutano huo. Kampuni ya Bia ya Mabibo imedhamini onesho hilo. Kulia ni Ofisa Mauzo wa Kampuni ya Bia ya Mabibo, Salumu Kabanda.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Na Mwandishi Wetu
MWANAMUZIKI mkongwe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Bileku Mpasi, atafanya onesho maalum katika utambulisho wa nyimbo mbili mpya za bendi ya Mashujaa

utakaofanyika Desemba 12 mwaka huu kwenye ukumbi wa Ten Lounge zamani Business Park.

Akizungumza Dar es Salaam leo mratibu wa onesho hilo, King Dodoo la Buche, alisema kuwa Mpasi ambaye alitamba katika tasnia ya muziki wa dansi alipokuwa na gwiji, marehemu, Pepe Kale, atakuja na wasanii wengine ili kutoa burudani ya kiwango cha juu.

Dodoo alitaja nyimbo hizo mbili ambazo zitatambulishwa ni pamoja na Rafiki Sokoni na My Queen.

Aliwataka mashabiki wa muziki wa dansi nchini kujiandaa kushuhudia onyesho hilo linalotarajiwa kuwa la kihistoria hapa nchini.

Rais wa Mashujaa Musica, Chalz Baba, alisema kuwa wamejiandaa kutoa burudani nzuri na kuendeleza heshima yao ya bendi bora kwa mwaka wa pili mfululizo.

" Napenda kuwahakikishia wapenzi wa bendi yetu tutafanya kazi ya ubora wa juu, ni kawaida yetu kufanya kazi nzuri, tuna usongo," alisema Chalz.

Katika onesho hilo lililodhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Mabibo kupitikia kinywaji chake cha Windhoek.

Akizungumza kwa niaba ya kampuni hiyo meneja biashara wa kampuni hiyo Joseph Emmanuel, alisema wameamua kudhamini utambulisho huo ili kuendeleza muziki wa dansi nchini kufikia hadhi ya kimataifa.

Alisema kuwa wapenzi 100 wa kwanza watakaoingia kwenye onesho hilo watapewa bia moja ya Windhoek Draught bure.

Mashujaa pia itatumbuiza nyimbo zake zilizotamba katika albamu zake za Risasi Kidole na Ushamba Mzigo.

Naye Rais wa Mashujaa Chalz Baba amewataka wapenzi wajiandae kupata burudani ya aina yake katika uzinduzi. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

No comments: