Advertisements

Saturday, November 15, 2014

MHE. MWAKYEMBE AKUTANA NA BALOZI MDOGO WA TANZANIA, DUBAI, MHE. OMAR MJENGA

Waziri wa Uchukuzi Mhe. Harrisson Mwakyembe, amekutana na kufanya mazungumzo ofisini kwake na Mhe. Omar Mjenga, Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai.

Mhe. Mjenga amemueleza Mhe. Mwakyembe kuhusu mazungumzo yake pamoja na Mhe. Gaith Alghaith, Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la FlyDubai, kuhusu mpango wa shirika hilo kuingia makubaliano ya ushirikiano pamoja na shirika la Ndege la Tanzania(Air Tanzania) ambako Flydubai watatoa ndege tano zitakazochukua njia za ndani (domestic routes) na zile za kikanda (regional routes).

Ushirikiano huu utasaidia kufufua njia zote za ATC na kuiwezesha ATC kuanza kupata mapato.

Njia za kikanda ni pamoja na Kinshasa, Lubumbashi, Goma, Kigali, Bunjumbura, Entebe, Nairobi, Sychelles, Moroni, Madagascar, Mauritius, Maputo, Lilongwe, Lusaka, Joharnessburg, na Harare.


No comments: