Advertisements

Friday, November 28, 2014

MHESHIMIWA PROF. ANNA TIBAIJUKA BORA UJIUZULU KULINDA HESHIMA YAKO NA CHAMA

Mheshimiwa Bi.Anna Tibaijuka (Mb)

Na Projectus Ishengoma Lugumalila
Mheshimiwa Bi.Anna Tibaijuka (Mb) Waziri wa Ardhi ni moja wa viongozi wachache sana wenye ujasiri na kiongozi muwazi katika sakata zima la Tageta ESCROW,kwani kiongozi huyu amekili wazi kuwa amepokea fedha Billion 1.6 kutoka kwa mmiliki
wa kampuni ya VIP Engineering Bw.James Rugimalira,tena si fedha ndogo.

Si jambo jema kumuhukumu Mheshimiwa Anna Tibaijuka,lakini sio vibaya kumshauri kwa kuwa amekuwa muwazi katika sakata hili,basi lingekuwa jambo la maana sana kama angejiuzulu madaraka aliyonayo katika serikali ili kulinda heshima yake na ya chama tawala.

Msomi yoyote yule anapofikia ukiitwa Professor na tena waziri mwenye kushika dhamana ya nchi na wananchi yaani Ardhi na makazi, ardhi ndio kila kitu kwa watanzania,harafu akafikia sehem ya kukubali kupokea fedha ya kiasi kikubwa Shiling Billion 1.6 kutoka kwa mfanyibiashara ! naye Mhe.Anna Tibaijuka bila ya kutia shaka yoyote kama ananuliwa kwa namna moja au nyingine kutokana na dhamana ya cheo chake ? hapa kwa mtanzania yoyote haingii akilini. Litakuwa jambo bora kwa Mhe.Anna Tibaijuka kujiuzulu ili aonyeshe mfano bora kuwa yeye ni kiongozi mkweli na viongozi wengine watafuata nyao.

Tunajua mtu apoitwa Professor sio msomi wa kawaida bali msomi aliefikia daraja
la juu kabisa,ndio maana tunaona msomi kama kiongozi wetu huyu ambaye anajua wazi kuwa yeye ni mojawapo wa mawaziri wachache ambao wizara zao zina dhamana kubwa ya nchi, leo hii anakubali kununuliwa kiurahisi pia kufanya biashara akiwa katika madara mazito,kama atandelea kututumikia wananchi katika wizara ambayo pia inahusika na mipaka ya ardhi ya nchi,tuna mashaka nae.

Watanzania tunajiuliza hivi Mhe.Anna Tibaijuka yupo katika utumishi wa umma tena katika wizara muhimu na huku akiwa mkurugenzi wa mashirika au shule na miradi binafsi au? ndio kusema cheo chake cha utumishi wa umma ndio dhmana ya biashara zake ?
Hivi kuna hosptali ngapi hapa nchini azina dawa? je wakina mama wangapi wajawazito wanafariki wakati wa kujifungua kwa ukosefu wa vifaa vya mahosptalini? Shule ngapi ? za serikali ambazo azina madawati?
Leo Mheshimiwa ambaye tena ni Professor amepokea fedha Tsh.Billion 1.6 na kusema kuwa hakujua kama ni fedha chafu,watanzania tunamashaka nae.

Professor Anna Tibaijuka anafahamu wazi kuwa amevunja sheria ya maadili ya
viongozi wa umma " (Sheria namba13 ya mwaka 1995) ambayo inawataka viongozi watoe taarifa ya zawadi wanazopokea au malipo wanayolipwa".

Sisi wananchi wenye kuiamini serikali hii na juhudi za kiongozi wetu mhe. Rais DKT.Jakaya Kikwete (mungu amuongezee afya njema),hautuwezi kabisa kukubali au kuona kiongozi tena msomi Professor,anavunja dhamana ya wananchi na kumvunjia heshima mkuu wa nchi ambaye ndiye alikuteuwa.

Litakuwa jambo la busara sana Mhe.Anna Tibaijuka ujiuzulu ili kulinda heshima yako kama msomi Professor,pia kulinda heshima serikali na Chama tawala. Uwezi kutumikia ofisi mbili utumishi wa umma na biashara.

Wanachi tunasikitika sana kuona katika sakata la fedha za umma mpaka baadhi watumishi wa mungu ambao ni viongozi wa kanisa nao wanausika na bila ya uwoga wanapokea fedha bila ya hofu ya kujenga udini.

Mungu ibariki Tanzania,Mungu mzidishie afya njema kiongozi wetu raisi
Dkt.J.K

5 comments:

Anonymous said...

Kaka sasa wewe shule gani uliyoenda? huyu mama hajiuzulu kwa lipi?

Mzee aliyempa fedha hizo ni mhaya mfanya biashara mkubwa sana Tanzania, anayetoa michango mingi kusaidia watu, last year peke yake alitoa 6 billion shillings kwaajili ya chuo kikuu Tabora ( Catholic University - Bishop Mihayo).

Huyu Mzee ametajwa kwenye report kuwa ni yeye peke yake ndiye aliyepa kodi, na yule mhindi hajalipa chochote…sasa kama huyu mama alipokea mchango wa shule yake kosa lipo wapi?

Report ya ya mkaguzi wa mahesabu ambayo ni muhimu hajamtaja, report ya Zitto inasema kuwa amepokea pesa toka kwa huyo mzee mfanya biashara..sasa hili la kujiuluzu la wapi? tungoje Takukuru ndio tuone ukweli wote…ni wazo langu tu.

Anonymous said...

Hog wash! Aliyeandika hapo juu akidai haoni sababu ya the so called professor kujiuzuru ni typical of many in our country ambao tumekuwa so blind to ethical issues. Kimaadili tu ingepasa hata angalau asimame kando hadi atakapoonekana hana hatia. Ile tu kungngania mbele ya tuhuma mbaya kama hizi inadhihirisha udhaifu wa viongozi wetu na mfumo wetu mzima wa kiutawala. Ni aibu kwamba viongozi kama hawa na akina Chenge ni sehemu ya Utawala wa nchii yetu. Mwalimu must be turning in his grave! Hatma ya nchi yetu sijui itakuwaje!!

Anonymous said...

Kwako mtoa maoni namba 1,
Hivi katika maoni yako uoni kuwa ukweli wa habari hapo juu mwandishi katoa sababu tena nzito za Waziri Anna Tibaijuka kujiuzulu,kwa taarifa yako Prof.Anna Tibaijuka ametenda kosa akiwa madarakani katika cheo tena waziri wa Ardhi hawezi kuwa kibakuri cha kuombea misada ya miradi yake,kwani ? tuna shue ngapi hazina vifaa.hivi ukweli huu nao unafumbiwa macho kama kivuli cha udini na ukabila kilifunuka mgawao wa fedha za umma.unasema huyo mfanyi biashara kasaidia michangi mengi ya kijamii kama makanisani,mchango wa kanisa sio wa kijamii bali ni wa Kidini na hili nalo ni tatizo linaloibuka nchini kwetu wezi kutumia dini
ni vema Prof.Anna Tibaijuka ajiuzulu ili kupisha uchunguzi zaidi

Anonymous said...

Mh Tibaijuka. Usisikilize maneno ya watu yakakuvunja moyo. Tunaokufahamu tunajua wewe ni mtetzi wa wanyonge. Watoto wakike wasio na uwezo wamelimika kupitia mkono wako. Shirika la UN-Habitat ulivyojiunga ulikuta contributions za member states ni $30 million wakati unaondoka uli build trust na member states contribution iliongezeka to 150 million 500% increase. One of ur strength ni kufundraise. Tupo na wote mama wa wanyonge.

Anonymous said...

Nadhani nchi yetu wapo watu wengi kama huyo mtoa maoni namba moja ndy maana tupo nyuma kimaendeleo.Nakupa mfano mmoja tu kama unafahamu ile shule yake ameajili walimu toka Canada,England na South Africa na wanalipwa kidola.Na hapo nyumbani kunawalimu wangapi hawana hasira? Ni maoni yangu tu ukishakuwa mkuu yyt ni kioo cha jamii