ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, November 23, 2014

MWIGULU NCHEMBA ATEMA SUMU,WEZI WA ESCROW/IPTL WAKAMATWE,WAFILISIWE,WAFUNGWE.KUJIUZULU TU HAITOSHI.

Imenukuliwa Kutoka Gazeti la Mwananchi(www.mwananchi.co.tz)

Habari zaidi kutoka ndani ya kikao hicho zinaeleza kuwa Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba alitoa msimamo mkali kuhusu sakata hilo la escrow na kwamba ametaka hatua zichukuliwe kwa wahusika wote.
Katika kikao hicho inaelezwa kwamba Nchemba alionyesha msimamo wake waziwazi kuwa sakata hilo ni hujuma  na kwamba haiwezekani walioiba fedha hizo wakaachiwa tu hivihivi.
Ndani ya kikao hicho imeelezwa kuwa Mwigulu alijitokeza na kusema Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ameshamaliza utata hivyo, mali zote, fedha zote za IPTL zikamatwe na wahusika wote wakamatwe.
Alisema haiwezekani watu wakawajibika tu kwa kujiuzulu kwa kuwa huko ni kutoa tu likizo mtu akale mabilioni yake, hivyo wachukuliwe hatua ipasavyo na kufilisiwa.
“CAG ameshasema pesa zile zilikuwa mali ya umma, sasa zikamatwe zote na wahusika wote wakamatwe,” alisema Mwigulu.
Chanzo chetu cha habari kilieleza kuwa Mwigulu alienda mbali zaidi na kusema hata ambao walishastaafu na wamehusika kulihujumu taifa wakamatwe na akaunti zao zikamatwe, zifilisiwe na fedha zirudishwe kwa wananchi.
Pia aliagiza mtumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambaye anatuhumiwa kuchota Sh1.6 bilioni za akaunti hiyo afukuzwe kazi, akamatwe na akaunti zake za fedha zifilisiwe ili fedha irudi serikalini.
Habari za uhakika kutoka kikao hicho zinaeleza kuwa Mwigulu aliongea kwa sauti ya mamlaka mbele ya Waziri Mkuu na kusema kuwa kujiuzulu siyo adhabu stahiki kwa wizi mkubwa kama huo.
Mwigulu alisema: “Tazama wanafunzi, watoto wa maskini zaidi ya elfu 40 wamekosa mikopo, madawa hospitalini hakuna, maskini wanakufa, watu wasio na hatia wanafungwa kwa kukosa michango ya maabara, walimu wanadai fedha zao, wazabuni wanauziwa nyumba zao na benki huku wakiidai Serikali kwa huduma walizotoa, leo wezi tuwape adhabu ya kujiuzulu? Tuwape likizo ya kwenda kutumia fedha walizo waibia maskini?”
Kwa mtumishi wa TRA aliyekula fedha za IPTL zaidi ya 1.6 bilioni Mwigulu akatoa agizo:
“Nimemwagiza Kamishna wa Kodi amfukuze kazi yule mtumishi wa TRA iliyoko chini ya wizara yangu na afilisiwe, pia mitambo na kodi vikamatwe na wahusika wakamatwe.
“Hatuwezi kuendeleza mazoea ya kufunga maskini na kuwapa likizo wezi wakatumie fedha. Walio serikalini na walioko kwenye siasa wakamatwe na tuwafilisi fedha irudi serikalini,” Mwigulu alisisitiza.

4 comments:

Anonymous said...

We need 2 or 3 of the Mwigulus. Jamani we think gas and oil will save us, I doubt very much, hizo revenue zitaliwa na wajanja.

Anonymous said...

Go Mwigulu, we need you!!! Where have you been. TUSAIDIE KIJANA WETU, tunakuomba TUSAIDIE KIJANA WETU

Anonymous said...

Nafikiri bado kipindi cha kampeni ya nani atagombea uraisi wa Tanzania hakijaanza. Lakini napenda kuwakumbusha watanzania kuwa awamu ya kwanza chini ya mwalimu Julius Nyerere ilifanya kazi kubwa sana kubwa kumjali mtanzania awe wa hali ya chini ya kati hata wale waliokuwa na fedha kidogo benki baada ya kueleza wamezipatapataje

nasema kujali kwa vile serikali ilishughulikia matatizo ya wananchi ikiwemo kujenga mashule mahospitali viwanda nk pamoja na usimamizi wake. Aidha mambo hayo yaliendelea hadi awamu ya raisi Mwinyi hadi pale tulipomwita mzee Ruksa

Lakini ninachotaka kusema leo ni hatua ya Naibu waziri wa fedha Mchemba Mwigulu alivyojawa na ujasiri wa kusema kama baba kwenye kikao cha viongozi wa bunge na wabunge wa CCM na kuomba hatua kali za kisheria dhidi ya wezi wa mali ya umma hasa fedha kwenye akaunti ya Escrow kwamba sii wajiuzulu tu bali wafikishwe mahakamani na kutaifishiwa mali zao na kufunga akaunti zao za nje na ndani

Kama ni kampeni basi huyu Mwigulu tungemweka kwenye kundi la marehemu Edward M Sokoine aliyekemea uhujumu uchumi na huyu amesema sana kwa uchungu kiasi kwamba kama ni kile kipindi cha kupiga kura ya ndio au hapana kwenye urais nafikiri angepata kuza zote za ndio kutoka kwa makundi kadhaa ya watanzania

Huyu ndiye kiongozu anayefaa bila kuangalia itikadi ya chama chochote cha siasa kwamba ana uchungu na raslimali za mtanzania na kama maneno yangu yana heri basi namwombea Mungu ili dhamira yake isibadilike na asishawishiwe ili aweze kulifikisha Taifa hili mahali Mungu alipopanga kwani ni taifa lenye maziwa na asali

Nina imani kwa maneno yake fedha hizo zikirudishwa kwenye uchumi naye akapewa ridhaa na wananchi kuendelea kusimamia kama kiongozi sekta nyingine kama ardhi, maliasili na utalii, Elimu kodi na mapato yatokanayo na uwekezaji mafuta na gesi tutaona mabadiliko makubwa tofauti na matarijio yetu. Basi nafasi ya kwanza kugombea urais na akishinda tumpe miaka mitano ya majaribio na akishiishinda na kulete mageuzi tuliyotegemea watanzania tumdhibitishe kwa iliyobaki

Ni lazima kila mtanzania awe na uchungu na nchi yake ili kuleta maendeleo ya kweli
Mungu ibariki Tanzania na watu wake

Anonymous said...

Mwigulu unastahili kulitumikia taifa kwa nafasi Kubwa zaidi ya hii naamini Mh rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania atapima kwa nafasi yake wapi akuwwke kwani naamini wengi wanahitaji msaada wako