Mholanzi Mart Nooij
Beki wa zamani wa Yanga na African Lyon, Aboubakar Mtiro, ambaye sasa anaichezea Kagera Sugar, ameitwa katika kikosi cha timu ya Taifa (Taifa Stars) ambacho kitaingia kambini Jumatatu Novemba 10 kwa ajili ya kuelekea Swaziland kuwakabili wenyeji hao kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa.
Mtiro (29), ameitwa na Kocha Mkuu wa Stars, Mholanzi Mart Nooij ikiwa ni miaka nane imepita tangu aiitwe kuichezea Stars wakati huo ikinolewa na Mbrazil Marcio Maximo.
Kwa mara ya mwisho Mtiro kuichezea Stars ilikuwa 2006, lakini Nooij amemrejesha kikosini baada ya kuonesha kiwango kizuri katika mechi kati ya Kagera Sugar dhidi ya Yanga iliyofanyika Novemba Mosi, mwaka huu kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, kocha huyo akiwa akishuhudia mchezo huo.
Akitangaza kikosi chake jana, Nooij alisema ameita wachezaji 24 lakini wawili ambao ni mabeki, Nadir Haroub 'Cannavaro' wa Yanga na Aggrey Morris (Azam) atawatema baada ya mechi dhidi ya Swaziland kwa kuwa ni wa Zanzibar na kuanza maandalizi ya mashindano ya Kombe la Chalenji ambayo yanayoshirikisha nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Nooij alisema kuwa kikosi cha timu hiyo kitaondoka nchini Novemba 11 kuelekea Johannesburg, Afrika Kusini kuweka kambi ya muda wa siku mbili na baadaye kuelekea Swaziland kwa ajili ya mechi hiyo ya kimataifa itakayofanyika Novemba 15 mjini Mbabane.
"Timu itaweka kambi ya siku mbili Afrika Kusini, itakwenda Swaziland kucheza mechi hiyo ya kirafiki na itarejea tena Afrika Kusini kuweka kambi ya wiki moja kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Chalenji na itaondokea huko huko kwenda kwenye michuano hiyo," alisema Nooij.
Hata hivyo, Nooij alishindwa kuwataja majina wachezaji hao wa Stars aliowaita na Mkurugenzi wa Takwimu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Martin Chacha, aliyatangaza ambao ni Deogratius Munishi 'Dida' wa Yanga, Aishi Manula, Said Moradi, Shomary Kapombe (Azam), Oscar Joshua, Cannavaro, Kelvin Yondani (Yanga), Morris, Emmanuel Simwanda (African Lyon), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar) na Hassan Isihaka wa Simba.
Viungo walioitwa ni Erasto Nyoni, Himid Mao, Salum Aboubakar (Azam), Mwinyi Kazimoto (Al Makhiya), Amri Kiemba, Haroun Chanongo na Said Ndemla wote wa Simba.
Katika nafasi ya ushambuliaji walioutwa ni pamoja Simon Msuva, Mrisho Ngasa (Yanga), Thomas Ulimwengu, Mbwana Samatta (TP Mazembe) na Juma Luizio wa Zesco ya Zambia.
Stars itashuka dimbani kuikabili Swaziland ikiwa na kumbukumbu ya ushindi mnono wa mabao 4-1 iliopata dhidi ya Benin hapa nyumbani.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment