Diamond ambaye juzi usiku alikomba tuzo tatu za Channel O ambazo ni Most Gifted New Comer, Most Gifted Afropop na Most Gifted East kupitia wimbo wake wa Number One anataraji kupiga shoo jijini Washington DC kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Sheraton akiwa na crew yake ya Wasafi.
Diamond ambaye kwa sasa ndio yupo juu kwenye gemu la muziki wa Bongo Flava alizungumzia ujio wake Marekani kwenye video clip aliyoweka kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Vijimambo iliongea na maporomota wanaoratibu safari ya Diamond Marekaani kutaka kujua ratiba nzima ya Rais wa Wasafi nao wamesema Diamond kama ulivyomsikia mwenyewe kwenye clip yake ya Video anatarajiwa kufika Washington, DC siku ya Ijumaa December 5, 2014 na wakazidi kusisitiza kwamba hakutauzwa tiketi mlangoni kwa kuogopa usumbufu nunua tiketi mapema.
Katika uchunguzi wa Vijimambo inaonyesha wakina dada ndio wengi walionunua tiketi mpaka sasa na Watanzania majimbo nje ya DMV pia ni miongoni ya walionunua tiketi hizi na kuna uwezekano ukumbi usitoshe kutokana msanii mwenyewe kuwa na jina kubwa katika tasnia hii ya Bongo Flava.
Show ya Diamond ni moja tu kwa hiyo wahi tiketi yako mapema uone ni kwanini Diamond ndio msanii wa Tanzania anayekubalika kimataifa na yeye mwenyewe ameahidi kufanya show ya nguvu itayoacha historia nchini Marekani na itakua show yake ya kwanza kufanya mbele ya Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani. Wahi tiketi yako mapema.
No comments:
Post a Comment