ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, December 31, 2014

BAO LA TAMBWE LA ZUA TAFRANI SIMBA HUKO

Mshambuliaji raia wa Burundi, Amissi Tambwe.

Na Wilbert Molandi
BAO la dakika ya saba lililofungwa na mshambuliaji raia wa Burundi, Amissi Tambwe, limezua tafrani kwa mashabiki na viongozi wa klabu ya Simba.Mrundi huyo alifunga bao hilo katika mchezo wa nane wa Ligi Kuu Bara, dhidi ya Azam FC, uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2, uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ukiwa ni mchezo wake wa kwanza kuitumikia timu hiyo.
Tafrani kubwa iliibuka uwanjani hapo, mara baada ya Tambwe kufunga bao hilo kwa kichwa akiunganisha krosi safi ya kiungo mkabaji, Salum Telela, aliyeng’ara kwenye pambano hilo.

Mara baada ya kufunga bao hilo, kundi kubwa la mashabiki walivamia jukwaa kuu sehemu wanayokaa viongozi wa Simba na kuwashtumu huku wakihoji sababu ya kumuacha Tambwe akiwa bado ana uwezo mkubwa.

Katika jukwaa hilo, alikuwepo Makamu Mwenyekiti Geofrey Nyange ‘Kaburu’ na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya timu hiyo, Said Tully ambao walitulia kimya.“Nyie vipi sasa mnamkataa Tambwe mnatuletea wachezaji wa ajabu kwenye timu yetu, Tambwe alitakiwa kuendelea kuichezea Simba.

“Hivi inawezekana vipi mnamkata mfungaji bora wa msimu uliopita.
“Sisi hatutamzomea Tambwe, kwa sababu hakuna chochote alichokifanya kibaya, yeye alitaka kubaki kuichezea Simba,” alisikika mmoja wa mashabiki hao.

Tambwe aliachwa na Simba dakika za mwisho kwenye usajili wa dirisha dogo lililopita lakini Yanga wakamsajili na juzi aliwafungia bao muhimu.
CREDIT:GPL

No comments: