Sunday, December 7, 2014

MHESHIMIWA RAIS TUNAKUOMBEA KWA MUNGU UPONE HARAKA, TUKO NAWE KWA DUA NA SADAKA

Rais Jakaya Kikwete.

Mheshimiwa rais, kwa niaba ya watu wa Oman tuishio Tanzania na wenzetu waliopo Oman, tunakuombea Mungu akujalie uweze kupona haraka ili urejee katika majukumu yako na kuendeleza nchi kwa ‘speed’ yako kali MANSHALAH.
Siku zote utakumbukwa kwa maendeleo uliyoifanyia nchi yetu ya Tanzania na ushirikiano mzuri na nchi zote duniani.
Tunakuombea upone haraka na upate furaha na kuweza kuyakamilisha uliyotuwazia kwa ajili ya taifa.
Mafanikio mengi katika kipindi chako kifupi cha uongozi tumeyapata na kuyafurahia, Allah akujalie.


Yafuatayo ni baadhi ya mambo uliyoyatekeleza.
Barabara nchi nzima hasa kwetu Tabora hakika ni mji tulisahauliwa, ama wewe mheshimiwa rais umetupa zawadi ambayo hatuwezi kukusahau.
Maji safi kutoka Ziwa Victoria, mikoa ya maziwa tumepata – shukrani mheshimiwa.
Tabora ilikuwa ni ndoto ya ajabu kupata kiwanja cha ndege na barabara za lami kwa sababu wazawa wengi kutokaTabora waliopata madaraka makubwa tangu uhuru lakini hawakuifanyia chochote.

Katiba mpya tumepata.

Diospora imejulikana sana na kutia chachu ya Watanzania walioko nje kujuana.

Wawekezaji wengi wazalendo na wageni na matunda tunayaona vijana wanapata ajira.

Kukomesha mauaji ya walemavu hasa albino.

Kupambana na madawa ya kulevya.

Kupambana na mafisadi.

Zahanati nyingi zimejengwa, hasa vijijini.

Shule nyingi vijijini na mijini.

Uhusiano mzuri sana na nchi ya Oman na dunia kwa ujumla.

Changamoto zilizobakia kwako Mheshimiwa Rais
Kukomesha waharibifu wanaotumia silaha ikiwezekana kutumia jeshi maana wanazuia maendeleo na usalama wa wananchi.
Kuboresha kilimo ili pato la taifa liongezeke na kuweza kuwapa mishahara mizuri askari na idara zingine za serikali ili kupunguza rushwa kwa kuwa watakuwa na mishahara mizuri.
Kusaidia dispora kuwa na kiongozi kila nchi ili aweze kuwa mwakilishi kati bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuchangia maendeleo ya taifa.
Uraia pacha ni muhimu sana ukaangaliwa tena, ukiangalia nchi zote zilizoendelea duniani zimesaidiwa na uraia pacha na sivyo watu wanavyofikiria. Tukumbuke wosia wa Baba wa Taifa, Julius Nyerere hasa katika suala la ubaguzi. Hivyo ubaya kwa nchi unaweza kufanywa na mzalendo na siyo mgeni.
Rushwa ni changamoto kubwa sana kwa kuwa ndiyo adui wa haki na maendeleo.

Tunaomba uwasiliane na Nile au Arab TV ili kuwaomba TV za bongo ziweze kurushwa maana leo kuna Ethiopia, South Sudan na Djibout maana na Imani TV zitaleta changamoto mbili muhimu sana kwa utalii, zitaonyesha neema za Tanzania na kuwa kivutio.

Changamoto kwa wananchi Ili kumwezesha raisi kufanikisha malengo tunayomuomba ni lazima tujue hapa duniani Mwenyezi Mungu katuwekea KATIBA MBILI yaani moja ya peponi na nyingine motoni.

Katiba ya Peponi Mpende kiumbe yeyote yule kama vile binadamu, wanyama, ndege na wadudu kama unavyoipenda nafsi yako.
Katika maamuzi yako ya haki basi usiwe na rafiki, adui na ndugu maana watakushauri watakavyo wao na hivyo kujikuta unafanya mambo kinyume na katiba ya pepo na kuwalidhisha wao.
Kuwa mwadilifu kwa kufuata maamrisho ya Mungu.

Katiba ya Motoni
Penda nafsi yako na chukia nafsi za viumbe wote kama vile binadamu, wanyama, ndege na wadudu.
Katika maamuzi yako ya haki basi uwe na rafiki, adui na ndugu maana watakushauri watakavyo wao, hivyo kujikuta unafanya mambo kwa kufuata katiba ya motoni.
Poteza haki za wengine ili muhimu wewe upate yako ya dunia ni ambayo ni ya muda mfupi.
Mwisho kwa wananchi tujiulize, je ni muda gani wa kuishi hapa duniani wakati leo mwezi imekuwa kama wiki na wiki kama siku?
Kwa mheshimiwa rais kuijenga nchi na kuangalia wananchi milioni 40, ni muhimu sana tumsaidie ili aweze kutimiza malengo yake kwa urahisi, njia pekee tuwe waadilifu kuanzia majumbani hadi kwenye ngazi za juu.

Wasalamu,

Hamoud Nasser Al Balushi - Tabora
Abdulwahab Salum Al Balushi – Tabora
Wote safarini Oman
Phone: +968-9626 7125

No comments: