Advertisements

Wednesday, December 31, 2014

MOROGORO WASHEREKEA MKESHA WA MWAKA MPYA KWENYE MAFURIKO

Mvua kubwa zilizonyesha kwa muda mfupi mjini Morogoro zimesababisha mafuriko baadhi ya barabara kushindwa kupitika na maji kujaa katika baadhi ya maduka. 
Wakazi wa mji wa Morogoro wakizungumzia mafuriko hayo wamelalamikia miundombinu mibovu ya barabara kutokana na kuziba kwa mitaro ambapo wameitaka halmasauri ya mji wa Morogoro kuzibua mitaro hiyo huku baadhi ya wafanyabiashara wakilalamikia kupata hasara.
Katika hatua nyingine mto Kikundi uliopo mjini Morogoro umepoteza uelekeo na kumwaga maji katika soko kuu la mji wa Morogoro na kusababisha maji kujaa katika maduka huku baadhi ya magari yakiingia kwenye mitaro na baadhi ya bodaboda zikiwa na abiria zime zama katika maji na kulazimika kuvutwa.
Kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Morogoro Phimlemon Magesa akizungumzia alalamiko hayo ya wananchi hao amesema manispaa wanajitahidi kufanya usafi lakini tatizo liko kwa wananchi wenyewe kutupa taka kwenye mitaro na kusabisha mitaro hiyo kuziba na maji kupoteza ueleko na kujaa katika makazi ya wananchi.

via>> itv.co.tz

2 comments:

Anonymous said...

tezi dume naskia kagoma kuwahutubia watanzania kwa kuwapa mkono wa mwaka mpya anasema wanazoza sana(wanasema sana,wanachamba sana)tusiache kusema kwa nini ananini?

Anonymous said...

wahaya wanazidi kumtetea tibaijuba wakabila hawa wahaya mmmfyuuu.