ANGALIA LIVE NEWS

Friday, December 12, 2014

MSIMU WA MAFUA MAKALI MAREKANI


Habari kutoka  kituo cha 
kudhibiti magojwa nchini Marekani  “Center for Disease Control” ( CDC) 2014 -2015, inatufahamisha kuhusu kipindi cha mafua makali ( Severe FLU Season).
Kipindi hiki kilichotawaliwa  zaidi na virusi vya A H3N2,hujulikana  kwa kuleta homa kali, ongezeko la  wagojwa mahospitalini na hata vifo. CDC inatukumbushia umuhimu wa kila mmoja kupata Chanjo  ya Flu na  tiba ya haraka ya kupamba na  virusi (Anti-viral drugs  treatment)  hasa kwa watu walio na kinga hafifu.  Anti-viral drugs husemekana kuwa mahiri zaidi kati ya masaa 48 baada ya dalili za flu kujitokeza mwilini .
Mabadiliko ya virusi kimaumbile (genetic) huchangia kupunguza umahiri wa chanjo japo wengi  waliofanikiwa kupata chanjo huwa na maambukizi  afueni.   CDC imeongeza kusema, FLU ya kipindi hiki iliyotawaliwa na  Influenza A H3N2 ilitokea  miaka ya 2012-1213, 2007-2008 na 2003-2004  vipindi ambavyo viliongoza  kwa idadi ya vifo katika ya miaka 10 iliyopita.
NINI DALILI  ZA FLU
  • Kukohoa au kukwaruza kwa koo
  • Maumivu ya kichwa
  • Baridi
  • Kuumwa mwili au uchovu wa mwili
  • homa
  • Mafua ya maji au yenye  kubana
NANI YUU HATARINI
  • Watoto chini ya umri wa miaka 5, wazee kuanzia miaka 65
  • Asthma
  • Wejawazito
  • Wagojwa ya Kisukari,  Figo,Ini,Circle cell
  • Magojwa yenye kuleta mapungufu ya kinga mwilini saratani,HIV/AIDS,
  • Watu wanaotumia baadhi ya dawa kwa muda mrefu kama steroids


Story
NesiWangu.blogspot.com
Shukrani
http://www.cdc.gov/flu/about/season/
Image

No comments: