ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, December 23, 2014

POLISI WATUMIA MABOMU KUWATAWANYA MACHINGA WALIOANDAMANA JIJINI DAR LEO

Askari Polisi wakiwapakia baadhi ya Wafanyabiashara ndogo ndogo(MMACHINGA) walioleta vurugu maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam leo.
Mkazi wa jiji akisaidiwa na wasamalia wema baada ya kuzimia kutokana na kupatwa na mstuko baada ya Polisi kupiga Mabomu katika sakata hilo.
Mkazi wa jiji akisaidiwa na wasamalia wema baada ya kuzimia kutokana na kupatwa na mstuko baada ya Polisi kupiga Mabomu katika sakata hilo.
Baadhi ya Mashuhuda wakisaidia Mkazi huyo kuhakikisha anapelekwa katika kupata Huduma ya kwanza.
Msamaria akiwa na Mkazi huyo wa jijini baada ya purukushani za Machinga dhidi ya Polisi jijini Dar es Salaam leo.
Moto uliowashwa na machinga ukiwaka barabarani eneo la Kamata, Kariakoo jijini Dar leo.
Gari la zimamoto likiwasili eneo la kamata kuzima moto uliowashwa na machinga.
Zimamoto wakiwa kazini.
Mawe yaliyowekwa barabarani na machinga wakati wakiandamana kuelekea ofisi za jiji.
Wanausalama wakiwa eneo la tukio.
Wananchi wakishirikiana kuondoa mawe barabarani ili kuruhusu magari kuendelea na safari zake.

JESHI la Polisi jijini Dar limelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafanyabiashara ndogondogo maarufu kwa jina la Machinga waliokuwa wanaandamana kuelekea ofisi za jiji eneo la Kamata, Kariakoo jijini Dar es Salaam leo.

Machinga hao waliamua kuchoma matairi na kuweka mawe barabarani wakati wa maandamano hayo ambapo madai yao ni kuhusu unyanyasaji wanaofanyiwa na askari wa jiji ikiwemo kunyang'anywa mali zao.

(PICHA NA MAKONGORO OGING' / GPL)

No comments: