Advertisements

Tuesday, January 27, 2015

AZA YA THELUJI YASABABISHA WASAFARI WA NJIA YA ANGA KUKWAMA, MAOFISI NA SHULE KUFUNGWA NEW YORK, NA MASSACHUSETTS

 Hii ndiyo hali ilivyo pande za New York  na Massachusetts theluji ilivyoanguka na kusababisha shughuli nyingi kusimama theluji imefikia inch 12 kwa New York na Massachusetts ni inch 24.
 Barabara zilikuwa zimejaa theluji na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wakazi wamiji hii.

 Abiria walilala uwanjani baada ya ndege kusindwa kuruka na kutua kutokana na theluji iliyoambatana na upepo mkali.
 Hatma ya abiria hawa itajulikana leo kama watasafiri au waendelee kusubiri hatma ya safari zao.
 Ndege zimeshindwa kuruka na kutoa viwanja vya LaGuardia, JFK New York na Boston.
 Ungetamani kujua anachokiwaza huyu abiria hapa ni uwanja wa ndege baada ya kushindwa kusafiri.
 Waliletewa vitanda vya kulalia hili wajisikie wako nyumbani. 
 Polisi wakichukua ukodak na pia wakihakikisha usalama.
 Barabara ni nyeupe watu wachache kama huyu alionekana akiwahi nyumbani.
 Njia za train zikifungwa hili watu wasiingie kwavile usafiri ulisimamishwa hadi hapo hali itakavyo kuwa shwari.
Mama na mtoto wake juu ya theluji wakicheza.

No comments: