ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, January 7, 2015

MASHABIKI YANGA, SIMBA WAFANANISHA UFICHO WA MAPATO MTANI JEMBE SAWA NA ESCROW

Na Saleh Ally
NIMECHAMBUA mambo kadhaa kuhusiana na mechi ya Nani Mtani Jembe iliyowakutanisha watani, Simba wakashinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Yanga.
Mechi hiyo ya mwishoni mwa mwaka jana ilifana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar. Siku chache baadaye nikaanza kuhoji kuhusiana na mapato kwa kuwa hayakutangazwa, kwa nini ilikuwa siri?
Nilitaka kujua kuhusiana na mgawo na Yanga na Simba zilifaidikaje kwa kuwa inaonekana wadhamini wao, Bia ya Kilimanjaro, walichukua kiasi cha fedha. Swali likawa vipi wadhamini wahusike na kuchukua mapato? Sikupata jibu.
Safari hii, si mimi. Ni mashabiki wa soka waliopata nafasi ya kutoa maoni yao kupitia ujumbe mfupi. Wapo ambao wamethubutu kuita ukimya wa kutotaja mapato hayo ni sawa na ile kashfa iliyotawala vyombo vya habari nchini, Escrow.
Wapo waliosisitiza Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), wengine Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), wafanye juhudi kuhakikisha mapato yanatangazwa.


Nimepokea zaidi ya meseji elfu moja, lakini kwa kuchukua mmoja kwenda mwingine, hawa wachache wamepata nafasi ya kutoa maoni yao na nitaendelea kuwapa nafasi wengine pia kadiri nafasi itakavyopatikana:


Viongozi wa Afrika siyo kwenye michezo tu bali kila kona wanaweza kuchakachua, hapa kuna kulindana sana wala hawawezi kutoa majibu ya mapato ya Nani Mtani Jembe, kila mtu ameshajikatia chake.
Man Jack wa Dar- 0652 204442


Kiukweli jamaa wanazingua mpaka leo hatujui pesa za mapato ziko wapi, usichoke kaka, pambana mpaka tuupate ukweli.
Twahiri Omary wa Tandika-0784 680266


Kwanza nakupongeza kwa kuwa mkweli kwa kufuatilia suala hili, umekuwa mtu wa kwanza kuuliza juu ya mapato ya mechi hiyo tofauti na vyombo vingine vya habari, unachouliza ni haki yetu wapenzi wa soka.
Amiri Juma wa Tandika-0717 208711


Hata wakitoa bastola wang’ang’anie mpaka waseme ukweli, fedha kachukua nani? Hao ni Escrow wa soka.
Abubakar Hamidu wa Chamazi-0717449887


Tunataka kufahamu nani wanatuibia fedha zetu, klabu nazo watueleze, kama hawajapewa mapato ya mlangoni itakuwa haina maana ya kucheza mechi kama hizo.
Khamisi Omary wa Kitunda- 0773 064753


Napata hofu katika suala hili la mapato ya Nani Mtani Jembe, yaani ukiangalia kwa undani nahisi kuna ujanja umefanyika kati ya TBL, klabu na TFF, pambana kaka mpaka kieleweke.
Salum Makamba wa Kigogo-0716 884284


Ni kweli timu zetu zinanyonywa sana katika mapato ya mechi ya Nani Mtani Jembe.
John Kajembe wa Muheza- 0714 634545


Nionavyo, mgawo wa mechi hiyo umeliwa na baadhi ya viongozi wa juu wa soka, ndiyo maana hatupati majibu sahihi ya mapato hayo.
Hemed wa Turiani- 0755 513054


Kiukweli TFF ndiyo wanatakiwa kutupa majibu sahihi juu ya mapato yote yaliyopatikana kwenye mchezo huo.
Emmanuel Nyika wa Mbeya- 0754 431852


Sisi tutakuwa nyuma yako daima katika kukusapoti mpaka tujue hizo fedha zimesaidia nini katika sekta ya michezo hapa nchini.
Cheche Idd wa Morogoro-0657 380198


Nakuunga mkono katika hilo, tunaomba tujulishwe hiyo Escrow ya soka ni akina nani wanaisimamia.
Alberth Tezura- 0767-636317

Inabidi ifike kipindi klabu hizo mbili zichoke kuburuzwa, haiwezekani ziingie zaidi ya milioni 600 halafu timu zipewe milioni 7, hapo lazima tuhoji fedha zinaenda wapi.
Nimrodi wa Makambako-0759 564936


Naona fedha za Mtani Jembe kama zilishaliwa hata kabla ya mechi yenyewe.
Baba Rahman wa Mbezi Beach-0717 220051


Katika suala hili la TBL, naomba usichoke, lifuatilie na sisi hatutachoka kusoma makala zako.
Amiry wa Zanzibar-0715 083206


Yaani ikiwezekana twende wote huko TBL tukaulizie wote kuhusiana na sakata hilo, huu siyo muda wa kumuogopa mtu yeyote.
Abdu Kirobo wa Mbagala, Dar- 0713-923168


Komaa kaka mpaka tujue fedha hizo zimeenda wapi na kufanya nini na kwa faida ya nani?
Said wa Kigoma-0714 815641


Mimi napendekeza ikiwezekana hata tufanye maandamano tujue hizo fedha zimeenda wapi.
Jay Meli wa Dar-0785 304209


Naomba kuungana na wewe, hivi hata wanachama na mashabiki wa Yanga na Simba hawana macho na masikio katika hili suala la Nani Mtani Jembe?
Matemba wa Mwanza-0787 169802
CREDIT:SALEHJEMBE

No comments: