Advertisements

Tuesday, January 27, 2015

MAZIKO YA MSHAURI WA RAIS UTALII ZANZIBAR


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa tatu kulia) Rais Mstaafu wa Zanzibar Alhaj Dk.Amani Abeid Karume (kulia) na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhaj Balozi Seif Ali Iddi pamoja na Viongozi wengine na waislamu mbali mbali wakijumuika kwa pamoja kumswalia aliyekuwa Mshauri wa Rais wa Utalii Marehemu Issa Ahmed Othman katika Masjid Mahfoudh Mazizini, Marehemu alifariki juzi Nchini India na kuzikwa leo Kianga Wilaya ya Magharibi Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein, (katikati) Rais Mstaafu wa Zanzibar Alhaj Dk.Amani Abeid Karume, Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhaj Balozi Seif Ali Iddi pamoja na Viongozi mbali mbali na baadhi ya Waumini wa kiislamu wakijumuika kwa pamoja kumuombea dua baada ya kumswalia aliyekuwa Mshauri wa Rais wa Utalii Marehemu Issa Ahmed Othman katika Msikiti Masjid Mahfoudh Mazizini,Marehemu amezikwa leo Kijiji cha Kianga Wilaya ya Magharibi Unguja.
Baadhi ya Vijana na wananchi waliobeba Jeneza la Marehemu Issa Ahmed Othman aliyekuwa Mashauri wa Rais Utalii Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakiupeleka kuzikwa kijijini Kianga Wilaya ya magharibi Unguja leo jioni,marehemu alifariki juzi Nchini India ambako alikwenda kwa matibabu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhaj Balozi Seif Ali Iddi (katikati) pamoja na Viongozi wengine na waislamu mbali mbali wakijumuika kwa pamoja katika mazishi ya aliyekuwa Mshauri wa Rais wa Utalii Marehemu Issa Ahmed Othman katika Kijiji cha Kianga Wilaya ya Magharibi Unguja leo jioni. Picha na Ikulu.

No comments: