Advertisements

Saturday, January 24, 2015

Rais Kikwete afanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri


Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue akiongea na vyombo vya habari jioni hii.

Hatimaye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete Ametangaza mabadiliko katika baraza lake la Mawaziri

Rais Kikwete amewateua mawaziri wanane wapya pamoja na manaibu watano. Tangazo hilo lililotangazwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika Ikulu ya Rais Balozi 

Mabadiliko hayo yanajumuisha wadhfa wa Waziri wa Nishati na madini Prof Sospeter Muhongo ambae amejiuzulu mapema leo pamoja na wadhfa wa waziri wa Ardhi ambao nafasi hiyo iliachwa wazi baada ya kujiuzulu kwa Anna Tibaijuka.

Mawaziri hao wawili wanahusishwa na Kashfa ya ufisadi ambayo ilimshinikiza hata mwanasheria mkuu wa Serikali kujiuzulu

Rais Kikwete anatarajia kuwaapisha mawaziri hao wapya hii leo katika tangazo litakarorushwa hewani moja kwa moja na runinga ya taifa
Hii ndio listi ya Mawaziri ambao wanadhaniwa kubadilishiwa Wizara zao 

Mabadiliko ya Mawaziri Na WIZARA
Mawaziri mmoja amejiuzulu na mmoja kuachishwa kazi
i) Ardhi-Tibaijuka ameachishwa kazi
ii)Nishati na madini-Sospeter Muhongo amejuzulu
Walio teuliwa
1. George Simbachawene- Waziri Nishati
2.Mary Nagu-Waziri wa Nchi mawasiliano na Uratibu
3.Christopher Chiza-Waziri uwezeshaji na Uwekezaji
4.Halson Mwakyembe-Ushirikiano wa afrika mashariki
5.Lukuvi-Ardhi Nyumba na Makazi

6.Steven Wasira-Kilimo chakula na Ushirika
7.Samwel Sitta -Wizara ya Uchukuzi

8.Jenista Muhagama-Sera na uratibu wa Bunge

No comments: