Ustadh Hemed (mwenye kipaza sauti) akiongoza kisomo cha kumwombea Rashid Mkakile apone haraka kilichofanyika siku ya Jumamosi Januari 17, 2015 mjini Boston jimbo la Massachusetts, Rashid Mkakile (hayupo pichani) alipata stroke alipokua kikazi jimboni hapo na kumpelekea kulazwa katika hospitali ya Beth Israel Deaconess Medical Center tangia mwezi wa Oktoba 2014 na baadae kuendelea na mazoezi ya mama cheza (Physical therapy) na kumfanya kuendelea vizuri na kesho Jumapili atarejea Dallas atapokua akindelea na mazoezi ya mama cheza na tunaomba muendelee kumtia kwenye maombi na sala zeni za kila siku. Kulia ni Salum mmoja wa mkazi wa Massachusetts na kiongozi wa Jumuiya ya Watanzania jimbo hilo ambaye yeye na wenzake walikuwa mstari wa mbele katika kumsaidia Rashid Mkakile na kuhakikisha hayupo peke japo hapo Massachusetts ambapo Mkakile alikuwepo kwa kizazi sio jimbo analoishi.
Watanzania wa Massachusetts wakifanya kisomo cha kumwombea Rashid Mkakile aendelee kupata nafuu kilichofanyika siku ya Jumamosi Januari 17, 2015. mjini Boston jimbo la Massachusetts.
Kushooto n Mohammed Mkakile(mdogo wa Rashid), Rashid Mkakile na Eliud Mbowe wakifuatilia kisomo.
Ikota akifuatilia kisomo
Eddy akitoa shukurani kwa niaba ya Watanzania wa Massachusetts.
Rashid Mkakile akitoa shukurani zake kwa Watanzania wa Massachusetts kwa kuwa karibu nae kwa muda wote tangia siku ya kwanza ya maradhi yake.
Ikota nae akitoa shukurani kwa niaba ya familia ya Rashid Mkakile.
Mayor Mlima akitoa shukurani kwa niaba ya Watanzania wa DMV na Massachusetts.
Watanzania wa Massachusetts na baadhi kutoka Michigan na DMV wakijumuika pamoka kwenye kisomo cha kumwombea Rashid Mkakile aendelee kupata nafuu na hatimae kupona haraka.
Picha ya pamoja na Mkakile
Kwa picha zaidi Bofya soma zaidi
8 comments:
Mashallah Mwenyeezi Mungu azidi kuwajaalia moyo Wa Upendo inshallah,hili ni jambo la kheri.
mashallah mmependeza wenyewe ummati mohammad s.a.w. Allah akujaliyeni hivyo hivyo msikamane kwa shida na furaha msitengane popote pale mlipo ummati Mohammed s.a.w.
na mgonjwa Allah amuafu Allah ma amin.
mpwawa umependeza mwenyewe mashallah mungu akubarik sana kwa kutuwekea picha hizi.
mdau NY.
ninajiuliza swali, na hili sina ushahidi nalo, mgonjwa wetu ni kwamba alikuwa ni muislam na akabadili dini kuamini dini nyengine, iman, maombi vinaambatana na imani unayoiamini, hapa inakuwaje wadau?
wenyewe wee
hivi kwanini hatutaki kusoma na kufuata sunna za Mtume Muhammad Swala llahu alayhi was salaam kwa mwendo ulio sahihi. Mtume anasema hivi lililobora ni lile alilolifanya au kufanya mas-haba zake, wakati wa Mtume na wakati wa kuondoka kwake katika karne zilizokuwa bora tatu za mwanzo, Mtume alikuwa anahimiza kwenda kuwaangalia wagonjwa kwa kupata ujira na yeye pia alikuwa ni mwenye kwenda.
na unapokwenda kumuangalia mgonjwa ni kumuombea dua, laa baasa twahurun IN SHAA ALLAH,
Sasa haya mambo ya kukusanyika kwenye maholi wanawake na wanaume eti mnamuombea dua mgonjwa sio katika mafunzo ya dini yetu ya kiislam.ni uzushi na kila uzushi ni upotovu na kila upotovu ni motoni.
hizo hela mlizotumia si ingekuwa bora mkampa mgonjwa akafarijika mngepata thawabu au mkamtolea swadaqa kwa kumtilia nia kwa kuwasaidia maskini na mayatima.
Tusiwe tunafanya mambo kwa vile tunavyotaka sisi tuwe wenye kusoma na kwenda sambamba kwa kile tunachokisema.
mwambieni mgonjwa ajisomee hii dua
bismilahi maratatu ikisha a3udhubilahi waqudratihi min shaari maa ajidu wa uhaadhir mara saba.
dawa ni chungu najua wengine itakuwa kumeza taabu lakini jitahidi isukumize kooni ili upate kupoa.
TUMUOMBE MWENYEZI MUNGU ATUONGOZE KATIKA KUTAMBUA MAMBO.
Duwa imefanyika salama na imemaliza salama endeleeeni kuongea pumba zenu
Rashidi and ikota, nawatakia safari njema na mungu awasaidie katika kipindi hichi kigumu. You guys are fighters and an inspiration to all of us. God bless you
pole
Tuendeleze upendo wetu na tuache majungu. Dua wakati wowote na mahali popote inakubalika!
Post a Comment