Advertisements

Tuesday, January 27, 2015

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI NA NAIBU WAKE WAANZA KAZI RASMI

Meneja Mradi wa Kinyerezi I kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco), Simon Jilima (katikati) akielezea maendeleo ya mradi wa Kinyerezi I kwa Waziri wa Nishati na Madini Mhe. George Simbachawene (wapili kulia) na Naibu Waziri wa Wizara hiyo anaeshughulikia Nishati, Charles Mwijage (kulia), Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Ngosi Mwihava (kushoto) walipotembelea mradi huo jana baada ya kuanza kazi.
Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) Dk. James Mataragio (kushoto) akimueleza Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (wapili kushoto), Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Ngosi Mwihava na Naibu Waziri wa Wizara hiyo anaeshughulikia Nishati, Charles Mwijage (kulia) juu ya hatua iliyofikiwa ya ukamilishaji wa kituo cha kuchakata gesi cha Kinyerezi I pamoja na ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi jijini Dar es Salaam walipotembelea kituo hicho

Waziri wa Nishati na Madini Mhe. George Simbachawene na Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Nishati) Mhe. Charles Mwijage (katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini na wataalamu wa mradi wa kuchakata gesi wa Kinyerezi.

Waziri wa Nishati na Madini Mhe. George Simbachawene (kulia) akizungumza mara baada ya kumalizika kwa ziara. Wengine kutoka kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava, Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) Dk. James Mataragio na Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Nishati) Mhe. Charles Mwijage.


No comments: