ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, February 19, 2015

HII NDIYO YANGA NA MBIO ZA KUUSAKA UBIGWA KIMYA KIMYA TU UNAISOMA

Yanga imerejea kileleni Ligi Kuu Bara baada ya kuichapa Prisons ya Mbeya kwa mabao 3-0.
Ushindi huo umeifanya Yanga kufikisha pointi 48 dhidi ya Azam FC yenye 46 ambayo imelazimishwa sare ya bila mabao dhidi ya Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
Yanga imebuka na ushindi huo mnono kwenye Uwanja wa ugenini wa Sokoine jijini Mbeya ikiwa ni baada ya viungo wake Simon Msuva na Andrey Coutinho kufunga.
Msuva amepachika mabao mawili, huku Coutinho na kukamilisha idadi ya tatu bila dhidi ya kikosi cha David Mwamwaja ambaye alitamba leo ingekuwa kazi ngumu kwa Yanga.
Pamoja na kuwa ugenini, Yanga walitawala mchezo kwa vipindi vyote huku wakipoteza nafasi nyingi za kufunga.
Mara kadhaa, Prisons nao walijitutumua hata hivyo kwa dakika zote 90 walifanikiwa kufanya mashambulizi makali au makubwa matatu tu.
Kwa kipigo hicho, Prisons inaendelea kubaki mkiani ikiwa na pointi 11 hivyo kuwa katika wakati mgumu na hofu ya kuteremka daraja.

1 comment:

Anonymous said...

mganga wao mkali kama wa dangote,diamond.