Advertisements

Wednesday, February 18, 2015

LADY JAY DEE AFUNGUKA KUHUSU KUWA NA MTOTO!

Jide akiwa na Mokonyo (mtoto wa mdogo wake Dabo)Lady Jaydee ameendelea kujibu maswali ya mashabiki wake kupitia Instagram, na maswali mengine aliyokutana nayo ni kuhusu kama ana mtoto au ameasili mtoto ambaye huonekana kwenye kipindi chake cha ‘Diary Ya LadyJaydee’ kinachorushwa kupitia EATV. 
“SWALI: Una watoto wangapi?
JIBU : Sina mtoto wala watoto 

SWALI:Utazaa lini?
JIBU : Sijajua mpk sasa nitazaa lini, ila siku yoyote ile ikitokea naweza kuzaa 

SWALI: Kwanini huna mtoto /watoto?
JIBU : Sina mtoto /watoto sababu sijawapata, nikipata nitakuwa nao. 

SWALI: Tunaskia ume adopt mtoto ?
Na mtoto tunaekuona nae ni wa nani?
JIBU : Sija adopt mtoto, mtoto mnae muona ana shine like a star, ananiita Shangazi, ninaishi nae sbb ya ukaribu wa shule anayosoma ,Tunaishi wawili tu, mimi na yeye
Anaitwa “Mokonyo Yvonne Mbibo” Ni binti wa mdogo wangu @dabomtanzania 

SWALI: Tunaskia una mtoto mkubwa ulimzaa ukamuacha kijijini Shinyanga /Musoma
JIBU : Sina mtoto niliemuacha kijijini, sijawahi kuishi kijijini.
Sijawahi kuishi Musoma, kwetu ni Bunda na huwa naenda ikitokea misiba kuzika, sijawahi kuishi huko zaidi hata ya miezi 2 Shinyanga niliozaliwa ni mjini
Nilihama Shinyanga, kuja Dar es salaam nikiwa na miaka 11
Sijawahi kurudi kuishi huko tena zaidi ya kwenda kusalimia. 

SWALI: Tunaskia huzai, ulitoa kizazi ili ufanikiwe kifedha?
JIBU : Sijatoa kizazi na sifanyi kitu chochote unusual ili kupata mafanikio
Angalizo : Mwenyezi Mungu hadhihakiwi, so stop calling me names. …….Kesho anaijua yeye, lolote pia linaweza kutokea. Accept me the way I am”.

5 comments:

Anonymous said...

Watu waangalie na maswali ya kuuliza..mtu kashajibu hana mtt...unauliza zaidi yanini..Hapo kama mtu mzima unaelewa..Watu wajifunze kuwa na staha jmn...kha!!

Anonymous said...

uko juu lady jay d tena nakupenda na nakuamini ni ma star wengi kama wewe wanakichwa na kujiheshimu huna hata chembe ya unafiki na utoto utoto,you are truly a star lady jay d,umewakata makali yao kwa kuwambia mungu ndo ajuaye kesho yako that's so nice of you.
wandishi wa habari wengi wamekaa kidaku daku kwa vile wameshawazoe ma star vicheche na wenye kuuza sura na kutaka umaarufu wa cheap cheap.

nakuaminia lady jay d.

mungu awe na we daima milele amen.
salaam kutoka kwa marekani

Anonymous said...

Mhhh! Jifunzeni.kuuliza maswali.

Jay said...

Waandishi wa habari wa Tanzania ndiyo maana wanadharauliwa for they don't know how to censor questions. Mtu kitu binafsi anauliza tena bila filtering, eti anajiita mwandishi wa habari kweli?

Anonymous said...

Nakupenda kwa sababu unajihamini, wewe siyo kama wasanii wengine. Mungu akutie nguvu na endelea kumtegemea kwa kila jambo. Mtoto ni baraka kutoka kwa Mungu wasikusonge na maswali kwano wao ni Mungu? Love u.