Advertisements

Wednesday, February 18, 2015

ZAIDI YA WAFANYABIASHARA 100 KUTOKA MIKOA YA MBEYA,IRINGA,NJOMBE KUHUDHURIA MAONESHO NCHINI AFRIKA KUSINI

Makamu Mwenyekiti Chama cha wafanyabiashara wa Kilimo na Viwanda Mkoa wa Mbeya ( TCCIA)wa Kwanza kulia Ndugu Emire Mahinza akizungumza na waandishi wa habri juu ya safari hiyo akiwa pamoja na Makamu Rais wa TCCIA Tanzania wa Pili kulia Ndugu Julius Kaijage pamoja na Mkurugenzi wa Blue Bird Burue De Change ya jijiji Mbeya Ndugu Janko Ndigo

- See more at: http://jamiimoja.blogspot.com/2015/02/wafanyabiashara-zaidi-100-kutoka-mikoa.html#sthash.nKhTlXrj.dpuf

Mkurugenzi wa Blue Bird Burue De Change ya jijiji Mbeya Ndugu Janko Ndigo wa kwanza kushoto akizungumzia juu ya ushiriki wa kampuni ya yake juu ya ushiriki wa maonesho hayo
Makamu Rais wa TCCIA Tanzania Ndugu Julius Kaijage katikakati akizungumza juu maandalizi ya safari hiyo

Na Mwandishi wetu,Mbeya
ZAIDI ya wafanyabiashara 100 wadogo na wakubwa nchini, wanatarajia kwenda kuzulu Afrika ya kusini ikiwa na kuhudhuria maonesho ya biashara yajulikanayo kama Esther Land Show.

Maonesho hayo ya kitaifa yanatarajia kufanyika, April mwaka huu, katika mji wa Johnsburg Afrika ya kusini kwa udhamini wa kampuni ya Blue Bird Buleu De Change iliyopo Jijini Mbeya.

Akizungumza jijini mbeya, Mkurugenzi wa kampuni hiyo Janko Ndingo, alisema ziara hiyo imelenga kuwakutanisha wafanyabiashara wa Tanzania na nchi ya Afrika ya kusini katika kujengeana uwezo ikiwa na kutangaza fursa zilizomo kwenye maeneo yao.

“Mji wa Johnsburg umekuwa ukiendesha maonesho ya biashara kila mwaka katika Sikukuu ya Pasaka, hivyo baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakihudhuria maonesho haya lakini kwa mwaka huu tunataka kuwashirikisha wafanyabiashara wadogo ili nao wafike na kunufaika na fursa hiyo,”alisema.

Alisema, maonesho hayo yamejikita zaidi katika masuala ya matumizi ya mitambo mbalimbali kama vile mitambo ya kilimo,vifungashio pamoja na ile inayozalisha bidhaa zikiwa na kiwango cha ubora unaoendana na soko la kimataifa.

Alisema, Afrika kusini kumekuwa na soko kubwa la bidhaa za kitamudi na zao la tangawizi zinazozalishwa Tanzania hivyo ni vema wafanyabiashara wakatumia fursa hiyo kwenda kutafuta masoko na kuanza kusafirisha bidhaa hizo.

“kinachotakiwa kufanywa na wazalishaji ni kuhakikisha bidhaa zote zinakidhi kiwango cha ubora wa kimataifa,”alisema.

Aidha, alisema kuwa ziara hiyo inashirikisha wafanyabiashara wote wanaonesha nia ya kutaka kujifunza na kubadilika ili kuondoka na hali ya umaskini na kwamba safari hiyo itaanzia Mjini Mbeya kwa usafiri wa basi kupitia njia ya Zambia na kwa gharama nafuu.

Hata hivyo, alisema kuwa safari hiyo itakuwa ni ya kitalii zaidi kwani wafanyabiashara watapata fursa ya kutembelea maporomoko ya mto Zambezi yajulikanayo kama Victoria yaliyopo nchini Zambia na kwamba ziara hiyo itakuwa ya siku 13.

No comments: